Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB Bw. Imani Kajula (kushoto)
akitoa ufafanuzi wa promosheni mpya ya Ki-College zaidi kwa viongozi wa
vyuo vya elimu ya juu waliohudhuria uzinduzi huo wikiendi hii.
Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Idara ya wateja binafsi wa NMB Bw. Abdulmajid
Nsekela,(pili kushoto) Makamu wa Rais wa chuo cha DUCE, Bi. Kagema Ftain
na Makamu wa Rais wa Chuo cha Ardhi Bw. Stephen Mokare.
Viongozi
wa Vyuo mbali mbali vya elimu ya juu wakiwa kwenye picha ya pamoja na
wafanyakazi wa NMB wakati wa uzinduzi wa kampeni ya NMB Student Account
iitwayo Ki COLLEGE zaidi na NMB, hafla hiyo ilifanyika wikiendi hii
jijini Dar es Salaam.
………………………………………………….
NMB ndiyo Benki yenye mtandao
mpana wa matawi na ATM nyingi zaidi nchini na imekuwa kinara katika
ubunifu Tanzania kwa kuanzisha akaunti zinazokidhi matakwa ya wateja
mbalimbali. Kwa kutambua jambo hili mwaka 2007, Benki ya NMB ilianzisha
akaunti maalumu kwa ajili ya wanafunzi iitwayo NMB Student Account.
Akaunti hii ilianzishwa ili kuwawezesha wanafunzi kupata huduma za
kibenki kwa urahisi na unafuu zaidi.
Ki-COLLEGE zaidi na NMB ni
promosheni inayowawezesha wanafunzi wenye akaunti ya NMB Student Account
kupata nafasi ya kuingia kwenye droo na kujishindia Zawadi mablimbali
kama: iPad, Samsung Galaxy, Amana maradufu, flash disk, fulana za NMB,
taa inayotumia mionzi ya jua au amana maradufu. Ili uweze kuingia kwenye
droo na kupata nafasi ya kujishindia zawadi kwenye promosheni ya Ki
COLLEGE zaidi na NMB, fungua NMB Student Account, weka amana katika
akaunti yako, tumia au jiunge na NMB mobile .Ikiwa hujatumia akaunti
yako kawa muda mrefu tembelea tawi la NMB ili nawe ushiriki katika
promosheni hii ya ki-COLLEGE zaidi na NMB.
Pamoja na kampeni hii, wanafunzi
watakao fungua NMB Student Account wataendelea kufurahia huduma za NMB
Student Account kama: Kufungua akaunti kwa Sh. 10,000 tu (pamoja na NMB
ATM kadi),kujiunga na huduma ya NMB mobile bure kupata huduma ya ujumbe
mfupi kila utoapo fedha kwenye ATM ya NMB bure, kuchukua fedha hadi
Sh.1,000,000 kwenye NMB ATM kwa siku na kupata huduma kupitia matawi
zaidi ya 143 na NMB ATM zaidi ya 450 nchi nzima. Kampeni ya ki-COLLEGE zaidi na NMB iliyoanza rasmi Oktoba 1 itaendelea hadi Desemba 31, 2012.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)