MAANDAMANO YAKIPITA
MBELE YA MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA LINDI AMBAYE ALIMWAKILISHA WAZIRI
WA AFYA NA USTAWI WA JAMII DR.HUSSEIN MWINYI (MB) KATIKA SIKU YA AFYA YA
AKILI DUNIANI AMBAPO KITAIFA IMEFANYIKA MKOANI LINDI KWENYE VIWANJA VYA
ILULU.
KWENYE BANDA LA NHIF
MGENI RASMI AKITOA RAI KWA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA KUONGEZA KASI
YA UHAMASISHAJI WA WANANCHI WA MKOA WA LINDI KUJIUNGA NA CHF,ILI
WAPATE UHAKIKA WA MATIBABU.
MWAKILISHI WA NHIF
MKOA WA LINDI FORTUNATA RAYMOND AKITOA MAELEZO YA MIKAKATI YA OFISI YAKE
KUHUSU MABORESHO YA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA MKOA WA LINDI NA
UHAMASISHAJI WA CHF KWA MKUU WA MKOA WA LINDI LUDOVICK MWANANZILA
ALIPOTEMBELEA BANDA LA MFUKO HUO KWENYE KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU
YA AFYA YA AKILI DUNIANI.
MGENI RASMI AKITIA SAHIHI KWENYE KITABU CHA WAGENI,ANAYESHUHUDIA KUSHOTO NI MENEJA WA NHIF KANDA YA KUSINI JOYCE SUMBWE .
HAKIKISHENI
UHAMASISHAJI WA CHF UNAWAFIKIA WALENGWA HUSUSANI WALIOPO VIJIJINI-RC LINDI
Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya ofisi ya Lindi umeshiriki kwenye maadhimisho ya siku ya afya ya
akili dunia kitaifa yamefanyika Mkoani Lindi mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Ludovick Mwananzila ambaye alimwakilisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii kauli
mbiu kwa mwaka huu ni… Sonona Ni Janga
La Dunia kwenye viwanja vya Ilulu.
Katika maadhimisho
hayo Mfuko umeshiriki kwa kutoa elimu kupitia banda lao kuhusu dhana ya
serikali kuanzisha na uratibu wa Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) ili wananchi
walio wengi wahamasike kujiunga na pia maboresho ya mafao mbalimbali
yanayoendelea kutekelezwa na NHIF kwa wadau na wanachama wake
Mkuu wa Mkoa
wa Lindi aliwataka Nhif kujikita zaidi kwenye uhamasishaji zaidi hususani
maeneo ya vijijini ambapo mahitaji ya huduma za afya kwa wananchi walio wengi
yako huko
…hakikisheni
kasi ya uhamasishaji inaongezeka na wanachi
wengi wanajiunga kwenye mfuko huu wa chf,haiwezekani kwa mkoa wa Lindi
uwe na wanachama asilimia 5.4 % ya kaya 194,424 ,hii ni ishara tosha kuwa
wananchi hawajapata elimu ya dhana na umuhimu wa mfuko huu katika kupata uhakika wa
matibabu,kwani hata kukosekana kwa fedha za
tiba unaweza ukawa chanzo cha
sonona miongoni mwa wanajamii..alisema mkuu huyo wa mkoa wa
Lindi Ludovick Mwananzila
amewataka mfuko kujipanga vyema kukabiliana na
changamoto za huduma za matibabu
zilizopo kwenye mkoa hususani uhaba wa dawa katika vituo vya matibabu,na
pale mtakapohitaji ushirikishwaji wa
ofisi yangu kwenye mpango wa uhamasishaji wananchi kujiunga na chf,ofisi yangu
iko tayari.alisema Mkuu wa mkoa
akizungumza
wakati wa maadhimisho hayo mwakilishi wa ofisi ya Mkoa wa Lindi Fortunata
Kulaya alisema changamoto kubwa iko kwenye matumizi ya fedha za tele kwa tele
na zinazolipwa na nhif kutokutumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa hivyo
kudhoofisha mwitikio wa wananchi kujiunga na chf.
Mfuko umekuwa
kwenye mkakati wa kuzishauri kamati na bodi za
afya zilizopo kwenye hospitali za mkoa,wilaya na vituo vya kutolea
huduma za matibabu kwa halmashauri zote zilizopo mkoani lindi,kuibua vyanzo
mbadala vya kununua madawa kupitia malipo ya tele kwa tele ili wananchi wanapohitaji huduma hiyo
ipatikane papo hapo.alisema kulaya
Alisistiza utaratibu usambazaji dawa uliopo una
changamoto zake lakini pia mfuko umeweka utaratibu wa mikopo ya vifaa tiba na
ukarabati wa majengo ili halmashauri zikope kwa kuboresha huduma kwenye maeneo hayo.
Pia aliwataka
wananchi kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhamasisha wananchi kufahamu
vyema madhara yanayosababisha sonona kwani tutakuwa tunajenga taifa lisilokuwa
na wabunifu wa maendeleo kwani afya ya akili ni ya msingi na kila mwanajamii
lazima awe nayo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)