Naibu Waziri wa Katiba na Sheria afanya ziara Gereza la Keko - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria afanya ziara Gereza la Keko

 Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela Kairuki akiwasalimia Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakati alipofanya ziara ya kikazi leo katika Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela Kairuki akionja chakula cha Mahabusu na Wafungwa wa Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam alipotembelea sehemu ya jiko la Mahabusu na Wafungwa gerezani hapo leo.
 Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akimkaribisha Naibu wa Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela Kairuki (wa pili kushoto) azungumze na Maofisa wa Magereza katika ziara ya Kikazi aliyoifanya leo Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Angela Kairuki akizungumza na Mahabusu na Wafungwa (hawapo pichani) wa Gereza la Keko jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo leo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages