Msamaria
mwema aliyrfahamika kwa jina moja Lina akiwa amembeba mtoto ambaye
alikutwa ametupwa katika bomba la Nyumba moja wilayani Sengerema.
Mtoto ambaye alitupwa akionekana katika picha..
Umati
wa watu waliofika kwenye tukio la utupwaji wa mtoto mchanga wakishangaa
sana kutokana unyama huo ambao haukubaliki kwa jamii ya Kitanzania.
-->
Sura ya Mtoto aliyetupwa kama inavyoonekana pichani.
NA PAULINA E. MPIWA SENGEREMA
MTOTO
mchanga anayekadiliwa kuwa na umri wa mwezi mmoja amekutwa ametupwa
kwenye boma la nyumba moja iliyopo katika kata ya Ibisabageni wilayani
sengerema mkoani mwanza.
Tukio
hilo limetokea jumatatu majira ya asubuhi katika kata hiyo ambapo mtoto
huyo amekutwa ametupwa na msamalia mwema ambaye ni mtoto aliyefahamika
kwa jina la KUBUNGA na kuamua kutoa taarifa kwa ndugu jamaa na ndipo
walipofika eneo la tukio.
Akielezea
kuhusu tukio hilo amesema kuwa wakati anapita eneo hilo alisikia sauti
ya mtoto ikilia na ndipo aliposogea karibu na kukuta mtoto huyo mchanga
akiwa amelazwa chini.
Naye
Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bw. JAPHET MASHALA ambaye alikuwepo eneo
la tukio amelaani kitendo hicho na kusema ni cha kinyama na kuwaomba
wananchi kuwa na moyo wa ubinadamu wa kuthamini maisha ya wengine kwani
mtoto huyo hana hatia yoyote.
Hata
hivyo mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio juhudi za kumtafuta
aliyetenda unyama huo zilikuwa zinaendelea ili kumfikisha katika vyombo
vya dola. Chanzo: B Plus Blog
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)