Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Yahana
Budeba akifungua mkutano wa wadau kutathmini maendeleo ya ya
Uvuvi, Wanyamapori, Misitu na Mifugo leo jijini Dar es salaam. Mkutano
huo uliowahusisha pia wadau kutoka nchi wafadhiri wa miradi ya maendeleo
na wadau kutoka asasi za kiraia unalenga kuimarisha usimamizi wa
maliasili na kupeleka madaraka ya usimamizi ngazi za vijiji.
Washiriki wa mkutano wa tathmini ya maendeleo ya sekta ya Uvuvi, Wanyamapori, Misitu na Mifugo wakijadili masuala mbalimbali kuhusu usimamizi endelevu wa maliasili zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mkutano kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wadau kutoka asasi za kiraia
zinazoshughulika na uhifadhi wa mazingira na washirika wa maendeleo
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt.
Yahana Budeba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu maendeleo
ya sekta ya Uvuvi, Misitu na Wanyamapori na hatua ya serikali ya
kupeleka madaraka ya usimamizi wa maliasili katika ngazi ya kijiji.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.









No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)