Mwenyekiti
wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami (kulia)
akiongea na waandishi wa habari (leo) jijini Dar es salam juu ya
Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi ya
Mashariki mwa Afrika unaofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza na
unaotarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Mohamed
Gharib Bilal . Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti wa TWCC Anna Matinde.
Mkutano huo unafunguliwa tarehe 22.10.2012 katika Hotel Kunduchi Beach.
…………………………………………………………….
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt.
Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa
Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi ya
Mashariki mwa Afrika unaonza kesho jijini Dar es salaam kwa lengo la
kuimarisha mtandao wao.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami
wakati akiongea na waandishi wa habari Ofisi kwake.
Amesema kuwa Mkutano huo ambao ni
wa saba(7) unafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu
walipoanzisha ushirikiano huo wa wanawake wafanyabiashara kwa nchi za
Afrika Mashariki.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa
wajumbe wa Mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika Nchi za Kenya, Uganda,
Rwanda , Burundi, Ethiopia , Sudan Kusini na mwenyeji Tanzania.
Amesema kuwa Mkutano huo utakuwa
fursa nzuri kwa wajumbe kutoka nchi zote saba kubadilishana uzoefu
katika kazi ya kuwainua kiuchumi wakimama na kuimarisha Mtandao wa
Wafanyabiashara wanawake katika Nchi za Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa hatua hiyo
itasaidia kufanya soko la wafanyabiasha wanawake wa Afrika Mashariki
kuwa kubwa na hivyo kuwainua kiuchumi wakimama.
Aidha Bibi Fatma Riyami amesema
kuwa TWCC imeanzisha matawi katika Mikoa ya Kagera, Mwanza, Pwani,
Dodoma, Mbeya, Dar es salaam na Arusha ikiwa na lengo la kutaka kuwa
karibu na wafanfanyabiashara wanawake kwa nia kuimarisha Umoja wao.
Wakati huo Mwenyekiti huyo
amewasisitiza wajumbe wa Mkutano huo kufika katika Hoteli hiyo ifikapo
saa 1.30 Asubuhi , Mgeni rasmi atafungua mkutano huo saa 2.00 kamili
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)