Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa CCM Mkoa wa Dar es
Salaam, Ramadhan Madabida, baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika
jana Oktoba 13, 2012 kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba na kutangazwa mshindi
katika kinyang’anyiri hicho kwa kupata jumla ya kura 310, huku mpinzani wake J.
Guninita akipata kura 214
Baadhi ya mashabiki wa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa
Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na wanachama wa CCM, wakishangilia na
kufurahia baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi
Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Madabida, akizungumza baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika
jana Oktoba 13, 2012 kwenye ukumbi wa PTA, jijini.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo
na Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, baada ya
Mwenyekiti huyo kutangazwa rasmi kushika nafasi hiyo kwa kumshinda mpinzani
wake, J. Guninita kwa kura 310 kwa 214, katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba
13, kwenye ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Madabida (kulia) akipongezwa na
aliyekuwa mgombea mwenzake katika kinyang’anyiro cha uchaguzi , huo, J.
Guninita, baada ya kutangazwa matokeo na kumsinda kwa jumla ya kura 310 kwa
214, katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa PTA jana Oktoba 13, 2012
Baadhi ya wanachama wapiga kura waliohudhuria
uchaguzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, akipiga
kura
Wasimamizi wa uchaguzi huo wakiwa bize kuandaa
utaratibu.Picha na OMR














No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)