Mtaalam
wa Mazingira wa UNDP Bw. Amani Ngusaro akitaja baadhi ya vikwazo
vinavyo kwamisha uboreshaji wa Mazingira katika maeneo ya makazi ikiwemo
uhaba wa maji na kutaka vikwazo hivyo viangaliwe upya na kuboreshwa
sambamba na kutolewa kwa elimu ya Mazingira na uhamasishaji katika ngazi
zote.
Amefafanua
kuwa hata katika utekelezaji wa sera za serikali kama vile Kilimo
Kwanza elimu ya matumizi sahihi ya Ardhi inapaswa kutolewa kwa wakulima
ili utekelezaji wa sera hizo uwe na tija na ufanisi zaidi kwa manufaa ya
taifa.
Afisa
Misitu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Freddy Manyika akitoa
nasaha zake kwa kusema kuwa sisi wananchi ndio tunatakiwa kuwa wa kwanza
kufanya mabadiliko na sio kuilaumu serikali kwani ndio tunaozungukwa na
mazingira.
Aidha
pia ametumia nafasi hiyo kutangaza kuwa suala la mabadiliko ya hali ya
hewa sio jambo la mzaha hivyo serikali inatakiwa kuwa na sera madhubuti
zitakazo wawezesha wananchi kukabiliana na madhara yatokanayo na janga
hilo ili kujitahidi kuirejesha ardhi na mazingira yetu kwa ujumla katika
hali bora.
Mtaalamu
wa Ikolojia Profesa Raphael Mwaliosi akitoa mada wakati wa majadiliano
ya hadhara yaliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa ikiwa ni Sehemu ya
Maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja huo ambapo amechambua changamoto baina
ya Mazingira na Mabadiliko ya hali ya Hewa hapa nchini na jitihada za
kukabiliana nazo.
Ameongeza
kuwa changamoto zaidi zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa
zinaleta athari mpaka katika Nyanja ya kiuchumi akitolea mfano sekta za
Kilimo, Maji, Nishati, Afya, Misitu, Uvuvi na Utalii.
Pichani
Juu na Chini Wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali jijini wakitoa
maoni yao katika mjadala wa wazi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee
ambapo wamelalamikia baadhi ya Sera za Serikali zisizotekelezeka wakatu
wa maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa kusheherekea miaka 67.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya Wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali
jijini waliohudhuria Mjadala wa wazi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa
katika kusheherekea miaka 67 tangu kuanzishwa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)