Katibu Tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement
Ndiomukama, akimkabidhi kitita cha Tsh.900,000 Nahodha wa timu ya Kabanga
Bushasha, Eliudi Prospa baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya
(Mitumbwi) Balimi Boat Race Wilayani
Bukoba Mkoani Kagera jana ambapo washiriki walishindana kuendesha mitumbwi kwa makasia.
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi
Boat Race) Mkoani Kagera upande wa
wanaume timu ya Kabanga Bushasha wanaume wakishangilia mara baada ya kuwa
mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki tisa (900,000) kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi
Boat Race) Mkoa wa Kagera upande wa wanawake Timu ya Seleka kutoka Musila,
wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya
shilingi laki saba (700,000) kama zawadi ya
ushindi wa kwanza.
Katibu tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement
Ndiamukama, akifungua mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race)
yaliyofanyika Wilayani Bukoba Mkoani Kagera ambapo zaaidi ya timu 50 zenye watu
watano kila timu zilishiriki, ambapo walishindana kupiga kasia kwa umbali wa
Kilometa 3 kwenda na kurudi, kushoto ni Meneja wa Mauzo wa Kanda ya Ziwa Endrew
Mbwambo na Afisa wa Sumatra Kapteni Alex Katama.
Meneja wa Bia ya Balimi Edith Bebwa(kulia)
akizungumza na washiriki wa mashindano ya Balimi Boat Race Wilayani Bukoba Mkoani
Kagera mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ambapo timu tano zitakwenda
kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali zitakazofanyika mkoani Mwanza Disemba mwaka
huu.
Waokoaji wakiwakoa wapiga kasia kinamama ambao walipinduka
Mabingwa Wanaumr Wakishangilia Baada Ya Kuwasili
WASHIRIKI wa shindano
la mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) ambayo ni maalum kwa mikoa ya kanda ya
ziwa wametakiwa kutumia pesa wanazozipata kwaajili ya kujiendeleza kwenye
miradi ya maendeleo.
Akizungumza mara
baada ya mashindano hayo Meneja wa Kinywaji hicho Cha Balimi Edith Bebwa,
alisema lengo la mashindano hayo ni kutoa shukrani na kuwawezesha wanywaji wake
hivyo wanapaswa kuzitumia kwenye kujiendeleza kwenye miradi yao.
“Nawaomba mlioshinda
na washiriki wengine ambao pia mmepata pesa hizo mzitumie kwenye miradi
yenu kama ni mvuvi basi ongeza chombo kingine au nyavu ili
mradi uzitumie kwenye uzalishaji” alisema Bebwa.
Awali akifungua
mashindano hayo Katibu Tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiamukama
aliwataka washiriki watakaoshinda kutobweteka na ubingwa badalayake wajipange
kwa mazoezi ili kwenye fainali ya mashindano hayo waupe heshima Mkoa wa Kagera.
“Tunataka mtuletee
heshima kwahiyo wale watakaoshinda watambue wajibu huo wakuletea heshima Mkoa,”
alisema Ndiomukama.
Mashindano hayo
ambayo yalianza Mkoani Kigoma October 27 mwaka huu yanatarajiwa kumalizika
kwenye fainali zitakazofanyika mwezi Disemba mwaka huu Mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)