Gwaride la wahitimu
wa Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili wakipita mbele ya Jukwaa la
Heshima kutoa heshima zao kwa mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Dk. Emmanuel Nchimbi.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akikagua gwaride la Wahitimu wa Mafunzo ya
Uongozi wa Magereza Daraja la Pili waliohitimu mafunzo yao katika Chuo cha Maafisa
Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Mafunzo
ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili waliohitimu mafunzo yao katika Chuo cha
Maafisa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam wakila kiapo cha utii kwa Rais na
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mhe. Jakaya Kikwete.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akimvisha Michael Mtimba Cheo cha Afisa
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Magereza, baada ya kuhitimu kozi ya uongozi daraja
la pili katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam
Kikundi cha ngoma
kikitumbuiza katika Sherehe za kufunga Mafunzo ya Uongozi wa Magereza katika
Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam.Picha Zote na Habari na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
----
Maafisa Magereza 153
wa Jeshi la Magereza nchini leo wamehitimu mafunzo ya Uongozi wa Magereza
Daraja la Pili katika Chuo cha Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi
waandamizi wa Magereza na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama ambapo Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi alikuwa mgeni rasmi. Kati ya
wahitimu hao, wanaume ni 102 na 51 wanawake.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)