KUTOKA VIWANJA VYA LEADERS KINONDONI FIESTA 2012 INAENDELEA USIKU HUU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KUTOKA VIWANJA VYA LEADERS KINONDONI FIESTA 2012 INAENDELEA USIKU HUU

Sasa ni zamu ya Lina wa THT akiwa jukwaani akiimba wimbo wake wa nampenda ambao umewafanya mashabiki wa muziki kuitikia kwa nguvu wakati akiwaimbisha hapa akipozi kwa staili ya aina yake huku akiwaimbisha mashabiki wake katika Tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku kuu kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambapo pamoja na wasanii mbalimbali wakali wa nyumbani, mwanamuziki maarufu wa Hiphop kutoka nchini Marekani Rick Ross “The Boss” atahitimisha tamasha hilo kwa shoo kali usiku huu.
Mwanamuziki Diana wa muziki wa Bongofleva kutoka kundi la THT akiimba katika Tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika usiku kuu kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam
Diana akibenwa juujuu na wacheza shoo wake wakati akifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Wadau kutoka kampuni ya bia ya Serengeti wakishoo love katika tamadsha hilo.
Mdau Edward na maiwaifu waki wakipozi kwa picha
Barnaba akikamua jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu.
Diana kutoka THT akimwaga mauno jukwaani wakati akiimba jukwaani usiku huu katika tamasha la Serengeti Fiesta.
Michael Jackson wa Bongo akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake alivuta hisia za wengi kutokana na kuigiza uchezaji wa marehemu Michael Jackson wa Marekani, pichani ni nyomi ya mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo kwenye viwanja vya Leaders
Msanii Aika kutoka kundi la muziki wa Bongofleva la Per One akifanya vitu vyake jukwaani katika shoo za utangulizi
Wasanii ha wa nao wamefanya mambo makubwa katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 usiku huu kwenye viwanja vya Leaders.
Kutoka kushoto ni Rachel, Lina na Daina wote kutoka THT wakiwa tayari kwa kazi ya kuburudisha mashabiki wa Tamasha la Serengeti Fiesa 2012.
Umakini kubwa kutoka kwa mashabiki kama wanavyoonekana katika picha
Mashabiki wakidatishwa na burudani za mwanzo za tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu kwenye viwanja vya Leaders.
Mtangazaji wa Clouds kipindi cha Amplifire Milad Ayo kulia akipozi kwa picha na mdau kutoka Gazeti la Babkubwa .
Msanii Aika kutoka kundi la Per One akifanya vitu vyake jukwaani na wasanii wenzake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages