KIM KUSHUHUDIA MECHI ZA LIGI KUU Z’BAR - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KIM KUSHUHUDIA MECHI ZA LIGI KUU Z’BAR

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Kim Poulsen (pichani) wikiendi hii ataanza ziara ya Zanzibar kuangalia Ligi Kuu ya Grand Malta kuwania ubingwa wa Zanzibar.
 
Kim anatarajia kushuhudia mechi zilizopungua tano akianzia kisiwani Pemba ambapo kati ya Oktoba 19 na 21 atashuhudiwa mechi mbili zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Gombani. Mechi hizo ni kati ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Grand Malta, Super Falcon ambao watacheza na vinara wa ligi hiyo Bandari, na baadaye mechi kati ya Duma na Bandari.
 
Baadaye atakwenda Unguja kwenye Uwanja wa Amaan ambapo baadhi ya mechi alizopanga kushuhudia ni kati ya Mtende na Chipukizi, Mundu na Jamhuri na KMKM dhidi ya Zimamoto.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages