Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akifungua kikao cha Bodi ya
Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam leo. Pamoja na mambo mengine amewataka
watendaji wa Halmashauri na Manispaa za jiji la Dar es salaam kusimamia
kikamilifu matumizi sahihi ya barabara ili kuondoa tatizo la msongamano
wa magari jijini Dar es salaam. Wengine wanaoonekana ni Mhe. Idd
Azzan(Mb) Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es salaam na
Michael Mungaya kaimu (kulia) Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es
salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akifungua kikao cha Bodi ya
Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam leo. Pamoja na mambo mengine amewataka
watendaji wa Halmashauri na Manispaa za jiji la Dar es salaam kusimamia
kikamilifu matumizi sahihi ya barabara ili kuondoa tatizo la msongamano
wa magari jijini Dar es salaam. Wengine wanaoonekana ni Mhe. Idd
Azzan(Mb) Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es salaam na
Michael Mungaya kaimu (kulia) Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda akitoa ufafanuzi kwa
wajumbe wa kikao cha Bodi ya barabara kuhusu changamoto mbalimbali
zinazoikabili manispaa ya Kinondoni ikiwemo baadhi ya watu waliojenga
maeneo yasiyoruhusiwa kutumia vibaya uhuru wa mahakama kufungua kesi na
kukwamisha uendelezaji wa baadhi ya miradi ya barabara na ubomoaji wa
baadhi ya nyumba zilizojengwa kinyumme cha utaratibu jijini Dar es
salaam.
Mbunge
wa jimbo la Kawe (CHADEMA) akichangia katika kikao cha Bodi ya Barabara
ya mkoa wa Dar es salaam leo jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa
watendaji wa Halmashauri kusimamia ipasavyo makusanyo ya fedha ili
kuziwezesha Halmashauri kuboresha miundombinu jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya Temeke Bi. Magreth Nyalile akijibu baadhi
ya maswali yaliyoulizwa na washiriki wa kikao hicho wakiwemo wabunge
kuhusu hatua zinazochukuliwa na Halmashauri ya Temeke kujenga
miundombinu na maegesho yatakayotumiwa na malori yanayotoka bandarini
na kupunguza kero kwa watumiaji wengine wa barabara hizo kutokana na
kushindwa kupitika kutokana na msongamano wa malori hayo.(PICHA NA ARON MSIGWA WA MAELEZO)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)