Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akizungumza na
Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi na Ufatiliaji wa uwekaji miundombinu ya
Digital ZBC hafla iliofanyika katika Jengo la Wizara ya Habari Utamaduni
Utalii na Michezo Zanzibar.PICHA NA MAKAME MSHENGA-HABARI MAELEZO
ZANZIBAR.
…………………………………
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Habari Utamaduni ,Utalii na
Michezo imeiteuwa kampuni ya Agape Associates LTD kufanya kazi ya kuweka
miundombinu ya matangazo ya mfumo wa Digitali ili kuwahi tarehe ya
mwisho ya matangazo ya Analogi ambayo ni 31 Disemba mwaka huu kama
ilivyokubaliwa kwa nchi za Maziwa makuu.
Aidha
wizara imemteuwa Hassan Katetei Mdachi kutoka Kampuni ya Thornhead
Engineering System,kutoka nchini Kenya kuwa Mshauri elekezi katika
kufanikisha shughuli hiyo.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Habari Utamaduni ,Utalii na Michezo Saidi
Ali Mbaruok wakati alipokuwa akizindua Kikosi kazi kitakachosimamia
uwekaji wa miundo mbinu wa mtambo wa DIJITAL-ZBC huko Ofisini kwake
Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Katika
uzinduzi huo amesema amelazimika kuunda kamati kwani mfumo wa dijital
harakati zake ni kubwa na za muda mfupi kufikia lengo ,hivyo kamati hiyo
itafuatilia kwa karibu mahitaji ya dijital ili wananchi waweze
kufaidika na huduma zake kwa wakati.
Kamati
hiyo itakuwa na lengo la kufuatilia na kusimamia kwa karibu shughuli za
uwekaji wa mitambo ya dijital katika vituo vyote vya unguja na Pemba.
Waziri
Said Mbarouk amesema majukumu mengine ni pamoja na kusimamia utaratibu
utakao weza kupatikana Ving’amuzi pamoja na njia zitakazo weza
kurahisisha wananchi kuvipata kwa wakati pamoja na kuanda na kusimamia
upatikanaji wa mandhari kwakuzingatia misingi ya kibiashara ,mila ,silka
na hali ya ushindani iliopo .
Ameyataja
majukumu mengine ya Kamati hiyo kuwa ni pamoja na kubuni njia bora
zitakazo saidia mtandao wa dijital kufanya kazi kwa ufanisi na
kujitegemea.
Katika
uzinduzi huo Katibu Mkuu wa Wizira ya Habari Utamaduni Utalii na
Michezo Zanzibar Ali Saleh Mwinyikai aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa
Kamati hiyo yenye wajumbe 13.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)