Mgeni rasmi Kamanda wa kanda maalum ya kipolisi mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akimkabidhi cheti cha uanachama wa Fema Club Ivon John Mkurugenzi mtarajiwa wa Flavour Media Company katika mahafali yakuhitimu elimu ya kidato cha nne ya shule ya Sekondari ya Kibasili yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo, Familia yako inakutakia maandalizi mema ya mitihani ya kidato cha nne inayotarajiwa kuanza Oktoba 8 mwaka huu Mungu akutangulie ili uweze kufanya kwa utulivu na hatimaye upate mafanikio ya kuenedelea na kidato cha tano.
Kamanda Suleiman Kova akitoa nasaha zake kwa wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza elimu ya kidato cha nne wakati wa mahafali hayo shuleni hapi kulia ni kaimu mkuu wa Shule Mwalimu Masoi
Mgeni rasmi na meza kuu wakifuatyilia kwa karibu matukio yaliyokuwa yakiendelea katika mahafali hayo.
Ivon John akikata keki huku dada yake wa shule Hapy ambaye anaingia kidato cha sita mwaka ujao akimuangalia.
Ivon John akiwa katika picha na shangazi ake kulia ni Shangazi Tusekile na kushoto ni Shangazi Neema.
Ivon akipozi kwa picha na zawadi zake.
Vijana wa skauti kutoka shule ya sekondari ya Kibasila wakionyesha uwezo wao jinsi ya kupita kwenye kamba.
Kamanda Kova amewaasa wanafunzi hao
kuwa na nidhamu katika masomo yao kwani nidhamu ndiyo inayozaa mafanikio
yote katika maisha ya binadamu, usipokuwa na nidhamu hata ungekuwa na
akili ya kiwango gani bila nidhamu utashindwa tu, na hautaweza kupata
mafanikio yoyote.
Akaongeza
na kusema "kwa sasa ajira ni ngumu hivyo msisome kwa malengo ya
kuajiriwa someni kwa malengo ya kuwa wajasiriamali na kubuni zaidi
shughuli za kufanya kuliko kufikiria ajira kwani hivi sasa wapo wasomi
wengi ambao wako mtaani na digrii zao"
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)