Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na
Watoto, Mhe. Sophia Simba, mgeni rasmi wa TWENDE 2011, akiangalia bidhaa za
ubunifu zilizotengenezwa na wajasiriamali wabunifu wa hapa nchini katika Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE,
2011 viwanja
vya mnazi mmoja. Kulia ni meya wa Halmashauri ya wilaya ya Ilala Mhe. Jerry
Silaa pamoja na Musatafa Hassanali, mjasiriamali mbunifu
na muasisi wa TWENDE (kushoto).
1.
Mgeni rasmi wa TWENDE 2011, Mh. Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba akishangazwa kwa
umahiri na uzuri wa kazi za ubunifu za mmoja kati ya wajasiriamali wanawake walioshiriki
Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE,
2011 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es slaam.
Pembeni yake kulia ni Mh. Jerry Silaa, meya wa Halmashauri wa wilaya ya ilala,
na kushoto ni Musatafa Hassanali, mjasiriamali mbunifu na muasisi wa TWENDE.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dr.
Cyril Chami akipokea maelezo juu ya ubunifu uliotumika katika utengenezaji wa
bidhaa ya kiutamanaduni kutoka kwa mshiriki wa TWENDE, 2011 katika viwanja vya
manazi moja jijini Dar es salaam.
Washiriki wa TWENDE 2011, wakisalimiana
na Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami mara baada ya waziri huyo
kuwatembelea katika banda lao na
kujionea bidhaa wanazotengeneza.
----
·
TWENDE 2012 KUFANYIKA KWA
MWAKA WA TATU SASA
·
SEMINA NA MAONESHO YA TWENDE
NI KUANZIA TAREHE 18 HADI 20 YA MWEZI WA KUMI KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA
JIJINI DAR ES SALAAM.
·
WANAWAKE WAJASIRIAMALI
KUELIMIKA, KUUZA BIDHAA ZAO NA KUKUZA MTANDAO WA KIBIASHARA KUPITIA JUKWAA LA
WANAWAKE WAJASIRIAMALI TANZANIA- TWENDE
Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE linatarajia
kufanyika kuanzia tarehe 18 – 20 ya mwezi wa kumi 2012 katika viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es salaam.
TWENDE imekuwa ikifanyika
kila mwaka kwa mwaka watatu sasa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2010, lengo
likiwa ni kuwaleta pamoja wanawake wajasiriamali wadogo, wakubwa na wale
wanaochipukia ili kupata fursa ya kuuza, kuonesha na kujadili masuala ya
biashara kwa ujumla.
Sambamba
na hilo. TWENDE inalenga kusaidiana na serikali katika kutimiza malengo ya
milenia likiwemo lengo namba moja ambalo linalenga kuondoa umasikini, namba tatu
kutetea haki na fursa sawa kwa wanawake, lengo namba tano kuhamasisha afya ya
uzazi na lengo namba nane, ambayo ni kuendeleza uhusiano wa kudumu kwa ajili ya
maendeleo ya jamii. Pia TWENDE inalenga Kukuza uzalishaji kwa wanawake
wafanyabiashara na kukuza mgawanyiko wa masoko sambamba na muonekano wa
wafanyabiashara wanawake katika jamii.
Kwa upande wa mwaka huu TWENDE inatarajia kuwashirikisha wanawake
wajasiriamali wengi zaidi ambao wamekuwa wakifanya biashasha tofauti ili kuweza
kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi zaidi kibiashara.
Sambamba na semina bora zitakazotolewa kwa wanawake wote ambao watapata elimu
itakayotolewa wataalamu wa fani mbalimbali
Kwa miaka mitatu mfululizo TWENDE imekuwa ikitoa fursa
kwa wanawake wajasiriamali kukutana pamoja na kujadili mafanikio na changamoto
ambazo zimekuwa ni kikwazo cha wanawake wajasiriamali kutofikia malengo yao
kibiashara.
“Licha ya kwamba wanawake wengi wamejikita katika sekta
hii ya ujasiriamali, lakini bado wamekuwa wakikabiliawa na changamoto
mbalimbali zinazokwamisha kufikia malengo yao, ikiwemo elimu ya ujasiriamli na
upatikanaji wa mikopo, kwa hiyo ipo haja kwa wanawake kujijengea utaratibu wa
kushiriki katika fursa kama hizi zinazowajengea uwezo”. Alisema Saphia Ngalapi
Meneja Mradi wa TWENDE.
Zaidi ya Wanawake Wajasiriamali Wanawake 100 kutoka mikoa
mbalimbali ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani wanatarajai kushiriki katika
TWENDE mwaka huu, ampabo maonesho hayo yanakwenda sambamba na semina zitakazo
tolewa kwa wanawake wote bure, kwa wale watakaoshiriki katika maonesho, na hata
wale ambo watakuwa hawakupata frusa ya kuonesha na kuuza bidhaa zao.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)