DAR ES SALAAM, Tanzania
Viongozi mbalimbali
wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekutana na kutoa tamko la kuzuia waislamu kuacha
kuandamana mara moja.
Katika
taarifa ya waliyoitoa mapema leo asubuhi wakuu na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo wa dini
wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick, (picha ya chini) aliwatoa hofu
wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani
wamejipanga kulinda hali ya amani.
Akitoa tamko
hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kumekuwapo na taarifa za waumini wa Kiislamu
kuandamana na kufanya fujo mara baada ya swala ya Ijumaa na baadala yake
amewataka kuacha kufanya hivyo na warejee majumbani kwa amani na suala hilo
linashughulikiwa kisheria.
Hata hivyo
kwa upande wao viongozi wa dini waliokutana na Mkuu wa mkoa juu ya kutolea tamko hilo waliwaasa waumini
wote kutoingia mitaani na kuandamana kwani wakifanya hivyo ni kukiuka misingi
mbalimbali ya kisheria iliyopo kihalali
na watakapofanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi.
Sheikh Mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa bin Salum amewataka wakuu wa misikiti mkoa
wa Dar es Salaam kuwakataza waumini hao kufanya maandamano kwani kufanya hivyo
ni kukiuka misingi iliyopo.Aidha,
aliwaomba waumini warejee majumbani kwa
amani.
Askofu Makunda aliwataka watanzania
kuendelea kufuata misingi ya kiimani bila chuki wala kufanya fujo.
Kamanda
wa Polisi Kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova (pichani juu) alitoa onyo kali
kwa waislamu kuacha kufanya hivyo hii leo kwani kwa atakaekiuka atachukuliwa
hatua kali. Kova
aliwataka waumini kurejea majumbani mwao kwa amani bila kufanya maandamano na pia aliwataka wakazi wa jiji la Dar es
Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kupuuza tishio hilo la fujo
kutoka kwa waislamu.
“Jeshi
limejipanga kuakikisha hali ya amani na usalama inakuwepo hivyo taadhari kwa
waislamu kuacha kufanya maandamano mara moja” alisema Kova kwenye kikao hicho
ambacho kinaendelea hivi sasa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)