BAADHI YA WAFUASI WA SHEIKH PONDA WAKAMATWA WAKIANDAMANA JIJINI KITUO KIKUU CHA POLISI KATI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BAADHI YA WAFUASI WA SHEIKH PONDA WAKAMATWA WAKIANDAMANA JIJINI KITUO KIKUU CHA POLISI KATI

Mmoja wa wafuasi wa kikundi cha waislamu wenye imani kali akidhibitiwa na polisi mara baada ya kukamatwa leo katika kituo kikuu cha polisi Kati wakijaribu kuandamana ili kushinikiza kiongozi wao Katibu wa Taasisi za Kiislamu Shekh Ponda  Issa Ponda kuachiwa na jeshi la polisi mara baada ya kukamatwa jijini Dar es salaam kwa kudaiwa kusababisha vurugujijini Dar es salaam.Mwandamanaji mwingine akipelekwa katika kituo kikuu cha polisi kati jijini Dar es salaam leo mchana mara baada ya kukamatwa akiandamana
Mmoja wa wananchi akihojiwa na waandishi wa habari ili kutoa maoni yake mara baada ya maandamano hayo kutawanywa na polisi na baadhi ya waandamanaji kukamatwa leo mchana
Polisi wakiwa tayari kwa kudhibiti maandamano hayo katika kituo kikuu cha Reli ya kati  na karibu na  kituo cha polisi kati jijini Dar es salaam leo mchana.Picha Kwa Hisani ya Full Shangwe Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages