Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambae pia ni Katibu Tawala Msaidizi
Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla akiwakaribisha wageni
hao Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufanya mkutano huo muhimu kwa maendeleo
ya sekta ya mifugo mkoani Rukwa na Taifani kwa ujumla.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Moshi Chang'a ambae pia ni Mkuu wa Wilaya Mpya ya
Kalambo akitoa hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia
Stella Manyanya ambaye yupo safarini kikazi. Kushoto ni Kaimu Katibu
Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Winston Mleche ambae pia ni
Mkurugenzi wa huduma za mifugo nchini. Katika hotuba yake hiyo alielezea
changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi ikiwemo uimarishaji wa mifumo ya
usafirishaji, uchukuzi na mawasiliano, kuboresha miundombinu ya masoko
ya mifugo, kuendelea kuboresha aina ya mifugo na mifumo ya uzalishaji
mifugo, kuboresha taratibu za umiliki wa ardhi na kuzuia magonjwa
mbalimbali ya mifugo. Hata hivo Mkoa wa Rukwa umepiga hatua kubwa katika
kupambana na magonjwa hatarishi ya mifugo ambayo kwa sasa yapo kwa
kiwango kidogo sana.
Kutoka
kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa kitengo cha Uchumi na
Uzalishaji Ndugu Respitch Maengo na Katibu Tawala Msaidizi kitengo hicho
kutoka Mkoa jirani wa Katavi Ndugu Sesemkwa.
Baadhi
ya wadau wa Mkutano huo wakifuatilia mada tofauti ndani ya Ukumbi wa
Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kikao hicho kitadumu kwa muda wa
siku mbili ambapo maazimio mbalimbali yantegemewa kufikiwa kwa ajili ya
kufanikisha adhma hiyo ya kuufanya Mkoa wa Rukwa eneo huru la magonjwa
ya mifugo kuimarisha bishara ya mazao ya mifugo kimataifa.
Kutoka
kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa kitengo cha Uchumi na
Uzalishaji Ndugu Respitch Maengo na Katibu Tawala Msaidizi kitengo hicho
kutoka Mkoa jirani wa Katavi Ndugu Sesemkwa.
Picha
ya pamoja kati ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia Mkuu wa Wilaya
Mpya ya Kalambo Mhe. Moshi Chang'a na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya
Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Winston Mleche pamoja na wataalamu wa
Mifugo kutoka Mikoa ya Rukwa, Njombe, Katavi, Tabora, Mbeya, Singida,
Shinyanga, Mwanza, Kigoma, Iringa, Kagera, Mara, Simiyu na Geita katika
kikao kilichowashirikisha wataalamu hao katika kujadili mpango wa
kuanzishwa eneo huru la magonjwa ya mifugo katika Wilaya za Sumbawanga
na Nkasi Mkoani Rukwa kwa lengo la kuwezesha kufanyika kwa biashara ya
mifugo na mazao ya mifugo kwa kufuata vigezo na masharti ya kimataifa.Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)