Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda akisaini kitabu cha wageni
ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, kabla ya kuanza ziara yake ya siku 3
kutembelea Viwanda Mkoani humo.
Waziri
wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda akizungumza na Mwenyekiti wa
Bodi ya Ukanda wa Uwekezaji wa Kiuchumi wa Mkoa wa Tanga Bw Chris Chae.
Uwekezaji mkubwa unatarajiwa kuanza katika eneo hilo hivi karibuni.
Mashine
za kisasa za kusaga na kupanga unga katika Viwango mbali mbali zilizopo
katika Kiwanda cha Unga cha Pembe kilichopo Mkoani Tanga.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Dkt Abdallah Kigoda, yupo katika ziara ya kikazi ya siku tatu kutembelea Viwanda Mkoani Tanga. Ziara hiyo ni maalum kwa lengo la
kuvitembelea Viwanda ili kujionea utendaji wake na kuhimiza utendaji
zaidi kwa sekta hiyo yenye mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi, ajira na
pato la Taifa.
Katika siku ya kwanza ya ziara
hiyo, Dkt Kigoda ametembelea Viwanda vya Saruji Tanga na Athi River,
Kiwanda cha mifuko na maturubai cha Pee Pee, Kiwanda cha Unga wa ngano
cha Pembe na Ukanda huru wa Uwekezaji Kiuchumi wa Mkoa wa Tanga.
Katika maeneo yote hayo, Waziri
Kigoda amesifu juhudi za Uongozi wa Mkoa wa Tanga katika kufufua Viwanda
vya zamani, kuibua fursa zilizopo katika sekta hiyo kwa kuanzisha
Viwanda vipya pamoja na kampeni kubwa ya kuhimiza uwekezaji inayofanywa
na Mkoa huo.
Ameahidi jitihada zaidi zinafanywa
na serikali katika kuongeza ufanisi wa sekta za Nishati hasa
upatikanaji wa gesi na Umeme, miundo mbinu ya barabara, reli na bandari
na ushiriki wa asasi za fedha katika kutoa mitaji ili kuisaidia sekta ya
Viwanda kutoa mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa nchi.
Ziara hiyo ya Waziri Kigoda na wasaidizi wake kutoka Wizarani inaendelea jumapili hii kwa kutembelea Viwanda mbali mbali.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)