Wajumbe
wa Baraza la Taifa la Usalama barabarani wametembelea maeneo
mbalimbali ambayo yamekuwa yakitokea ajali mara kwa mara katika barabara
kuu ya Morogoro-Iringa-Mbeya na kupeana ushauri juu ya hatua za
kuchukua katika kupunguza ajali hizo.
Mmoja
wa wajumbe hao akitoa ushauri kwa kikosi cha Usalama barabarani mkoani
Iringa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa
Iringa, Salim 'Asas' Abri.
Kamanda
wa Trafiki Mkoa wa Iringa, Mrakibu wa Polisi, Pamphil Honono, (kulia)
akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani mkoa wa
Iringa, Salim ‘Asas’ Abri wakati wa ziara hiyo.
Lori
la mizigo lililosheheni mbao likiteremka mlima Kitonga hii leo. Askari
wa Usalama barabarani wametakiwa kuongeza doria katika mlima huo
kufuatia ajali za mara kwa mara zinazotokea kutokana na madereva
kuendesha magari kwa fujo bila kuzingatiafuata sheria za usalama
barabarani.
Mteremkona kona Mlima Kitonga.
Basi la Taqwa likiwa limehariba katika mlima Kitonga leo.
Wajumbe wa Baraza wakimpa maelekezo OCD wa Kilolo juu ya kudhibiti ajali katika mlima Kitonga.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga akichukua picha katika mlima kitonga
Wajumbe
wa Baraza la Wiki ya Nenda kwa Usalama wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya kukamilisha ziara yao ya kutembelea mliama Kitonga. Maadhimisho
ya wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa yanafanyika Mkoani Iringa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)