Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda awasili Mjini Colombo, Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa 58 wa CPA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda awasili Mjini Colombo, Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa 58 wa CPA

Spika wa Bunge Mhe. Makinda akiwasili katika hotel ya The Grand Cinnamon mara baada ya kushuka katika basi maalum lililomchukua yeye na ujumbe wake kutoka uwanja wa ndege mchini Colomo Sri Lanka
Afisa Dawati la CPA katika Bunge la Tanzania Ndg. Said Yakubu akimpokea Mhe. Spika mara baada ya kuwasili mjini Colombo Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa 58 wa CPA. Katikati ni kamimu Katibu wa CPA kanda ya Afrika na Mkuu wa Sehemu ya Itifaki na uhusiano wa Kimataifa kutoka Bunge la Tanzania Ndg. Dimitries Mgalami
Ndg. Dimitries Mgalami akimsindikiza Mhe. Spika katika hotel itakayofikia wakati wote wa Mkutano huo wa CPA
kamimu Katibu wa CPA kanda ya Afrika na Mkuu wa Sehemu ya Itifaki na uhusiano wa Kimataifa kutoka Bunge la Tanzania Ndg. Dimitries Mgalami akiteta jambo na Mhe. Spika mara baada ya kumpokea alipowasili Colombo Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa mwaka wa CPA unaofanyika Nchini humo kuanzaia tarehe 7 hadi 15 Septemba, 2012.
 Mjumbe wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Zitto Kabwe akiteta jambo na Mhe. Okupa Elijah kutoka Bunge la Uganda mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege colombo Sri lanka kuhudhuria mkutano wa 58 wa CPA. aliyeko pembeni ni Mbunge kutoka Uingereza.zote na Owen Mwandumbya wa Bunge
---
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda  amewasili Mjini Colombo nchini Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola Dunian (CPA). Mkutano huo wa mwaka unafanyika Nchini humo kuanzaia tarehe 7 hadi 15 Septemba, 2012, ambapo zaidi ya wabunge 1000 na Maspika wa Mabunge zaidi ya 80  kutoka nchi mbalimbali wananchama wa jumuiya ya Madola watahudhuria mkutano huo wa mwaka.

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo unaongozwa na Mhe. Spika ambaye pia ataongoza wabunge wengine kutoka tawi la CPA Tanzania ambo ni Mhe. Ziito Kabwe, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Beatriace Shelukindo, Mhe. Hamad Rashid Mohamad na Mhe. Muhonga Ruhanya ambapo jumla ya mada 9 zinatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika mkutano huo. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages