Rais
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni
Jenerali Samuel Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo
jijini Dar es salaam. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa
wazi na Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini
kwa Umri.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael
Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo
Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na walioapishwa leo.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya
Ulinzi na Maofisa wa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa leo mara baada ya
hafla fupi ya kuwaapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa JKT Meja
Jenerali Raphael Muhuga.
Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto)
akimweleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Kikwete (kulia) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.Wengine ni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati).
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel
Albert Ndomba akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa
leo jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Maofisa
waandamizi wanawake wa JWTZ leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kulia ni
Meja Jenerali Lilian Kingazi (Kulia) na Meja Jenerali Grace Mwakipunda
(kulia).
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)