Wajasiriamali
wakifanya " practical " ya kutengeneza sabuni ya maji kwa
vitendo mara baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa waalimu wa
ujasiriamali kutoka katika Asasi ya RafikiElimu Foundation.
Mwanafunzi
wa ujasiriamali akitengeneza sabuni ya unga mwenyewe mara
baada ya kupata maelekezo kutoka kwa waalimu wa ujasiriamali
kutoka RafikiELIMU Foundation.
Baadhi
ya wajasiriamali walio hudhuria katika Uzinduzi wa Mradi wa
Elimu Ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini uliofanyika leo
jijini Dar Es salaam.
Akiulezea mradi huu, mratibu msaidizi wa mradi huo alisema kuwa mradi huu upo katika awamu kuu mbili. Awamu ya kwanza itafanyika kuanzia tarehe 01 Septemba 2012 hadi tarehe 29 Septemba 2012, na utafanyika katika mikoa ya Dar Es salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Dodoma na Kilimanjaro, ambapo mbali na kutoa mafunzo ya ujasiriamali, asasi itatafuta vijana kumi na wawili kutoka katika hiyo mikoa saba kwa ajili ya kufanya kazi kama wajitoleaji " volunteers" katika awamu ya pili ya mradi itakayo anza rasmi tarehe 01 Novemba 2012 na kuchukua miaka miwili hadi Novemba 2014 ambapo ndipo itakapo kuwa tamati ya mradi huu.

Awamu
ya kwanza ya mradi huu inafanyika katika mikoa ya Dar Es salaam,
Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Dodoma, Mwanza na Mbeya. Jijini Dar Es
salaam, mafunzo yanafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 01 Septemba
2012 hadi tarehe 04 Septemba 2012 katika Shule ya Msingi Mlimani ,
iliyopo katika Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam... Ratiba kamili ya awamu ya
kwanza ya mafunzo haya ni kama ifuatavyo :
1. ARUSHA, MOSHI & MOROGORO : Mafunzo yatafanyika kuanzia tarehe 17 hadi 19 Septemba 2012.. Mwisho wa kujiandikisha katika " programme hii " kwa wakaazi wa ARUSHA, MOSHI na MOROGORO ni tarehe 15 Septemba 2012.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)