Home
Unlabelled
MWENGE WA UHURU WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA
MWENGE WA UHURU WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA
Wananchi wengi wa
Mkoa wa Rukwa waliohusika kuulaki Mwenge huo wa Uhuru kwani wengine walilazimika
kuhatarisha maisha yao kwa kupanda juu ya miti ili waweze kuuona Mwenge
huo.
Baadhi
ya wananchi Mkoani Rukwa waking'ang'ania kushika mwenge wa uhuru kabla ya Mwenge
huo kuondoka kuelekea kuanza mbio zake Mkoani Katavi hapo
jana.
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya kumaliza mbio zake Mkoani Rukwa
ambapo Jumla ya miradi 27 iliyogharimu zaidi ya bilioni 5 ilizinduliwa na
kuwekwa mawe ya msingi katika Mkoa wa Rukwa.
Mwenge wa Uhuru
ukipewa heshma ya mwisho kwa stali ya mchakamchaka kabla ya kukabidhiwa rasmi na
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi mara
baada ya kumaliza mbio zake mkoani humo jana, Wakijumuika kwenye gwaride hilo la
utii kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddy Kimanta, Kiongozi wa Mwenge
Kitaifa Capt. Honest Mwanossa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Jumla ya miradi 27 iliyogharimu zaidi ya bilioni 5 ilizinduliwa na kuwekwa mawe
ya msingi katika Mkoa wa Rukwa.
Kiongozi wa mbio za
Mwenge kitaifa Capt. Honest Erenest Mwanossa akiagana na viongozi wa Mkoa wa
Rukwa mara baada ya kukamilisha jukumu zito la kukimbiza mwenge katika Wilaya
tatu za Mkoa wa Rukwa ambazo ni Sumbawanga, Kalambo na Nkasi. Alieshikana nae
mkono na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson
Mashalla.
Wanafunzi wa Shule ya
Msingi Nkasi wakiwa wamebeba bango lililokuwa na ujumbe wa Mwenge wa Uhuru.
Ujumbe wa Mwenge wa mwaka huu kitaifa ni Mabadiliko ya Katiba Timiza Wajibu Toa
Maoni yako na Mapambano dhidi ya Ukimwi na Dawa za kulevya.
Muongozaji wa Blog ya
Rukwareview Mr. Temba (shoto) akishare Photo na Mkimbiza Mwenge kitaifa Ndugu
Kajia Godfrey kutoka Shinyanga kabla ya kumaliza mbio hizo Mkoani Rukwa
jana.Picha na Habari zimeletwa hapa na Hamza Temba- Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)
Lukaza Blog is a resources blog providing high quality articles with premium topics and well drafted. The main mission of Lukaza Blog is to provide the best quality articles which are relevance, original, truth and education materials designed and perfectlly to deliver best result for your knowledge and understanding of new things.
Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Mzee Emannuel Humba akionyesha tuzo yake aliyopewa na mfuko huo kwa kutambua...
Contact Form
About Me
Hello, my name is Josephat Lukaza. I've 12 years in Blogging and An Award Winner for the BEST Political Blog in African Bloggers Awards in 2015 Learn More →
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)