Mkuu
wa mkoa Chiku Gallawa akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama
wakitazama jiwe linalotenganishwa mpaka wa Kenya na Tanzania.
Mkuu
wa mkoa wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa akitazama mkaa ukiwa umewekwa kwenye maguni tayari kusafirishwa kupelekwa nchini Kenya hasa
katika mji wa Mombasa.
Askari
polisi wakimsindikiza kwenda kuaga kwa mkewe Mwenyekiti wa kijiji cha
Mwakijembe Bw. Francis Mtiambo aliyekamatwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga,
Luteni (mstaafu) Chiku Gallawa kufuatia kumtuhumu kushindwa kusimamia
rasilimali ya Taifa.
Na: Mashaka Mhando,Horohoro
MKUU
wa Mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa, amemkamata na kumweka
ndani Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mwakijembe kilichopo mpakani
mwa Kenya na Tanzania, Francis Mtiambo, kwa madai ya kushindwa kulinda
rasilimali za Taifa.
Mkuu
huyo wa mkoa wakati akimkamata mwenyekiti huyo alisema ana mweka
ndanikwa kushindwa kusimamia na kutekeleza agizo lake la kuzuia agizo
lake la kusimamisha uvunaji wa miti na uchomaji mkaa alilolitoa Julai
mwaka huu kufuatia baadhio ya watu kuiharibu misitu hasa katika wilaya
za Handeni na Kilindi kwa kisingizio cha kuandaa mashamba.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho, anatuhumiwa kwamba ameshindwa kusimamia zoezi la
ukataji wa miti aina ya mipingo ambayo imekuwa ikikatwa kwa wingi katika
kijiji hicho na kuchongwa vinyago vinavyouzwa nchi jirani ya Kenya
pamoja na ukataji wa miti ya mikarambati na mikumbulu ambayo inachomwa
mkaa na kuuzwa huko nje ya nchi.
Mkuu
huyo wa mkoa alifanya ziara ya ghafla na kamati yake ya ulinzi na
usalama kwenye wilaya Mkinga kukagua shughuli za uchomaji mkaa
unaofanywa mpakani ambapo alipita katika wilaya ya Kwale iliyopo nchini
Kenya alipopewa askari wawili wa Kenya aliongozana nao hadi katika
kijiji hicho cha Mwakijembe baada ya kukagua mawe yanayotenganisha mpaka
wa nchi hizio.
Akiwa
mpakani huko mkuu huyo wa mkoa alikagua jiwe lililoandikwa namba T13-3K
na jingine T17-1K, pia alisikitishwa na uharibifu mkubwa uliofanywa wa
ukataji wa miti na uchomaji wa mkaa katika eneo la mpaka wa Tanzania
huku miti ya sehemu ya Kenya ikiwa haijaguswa hatua ambayo inaonekana
kwamba Watazania wanahujumu miti upande wao lakini wenzao wa Kenya
wanatii sheria ya utunzaji wa maziongira.
Pia
alishuhudia baadhi ya magari ya Kenya yakiwa yamesheheni magunia ya
mkaa yakitokea upande wa Tanzania hatua ambayo ilimsikitisha ikiwemo
kushindwa kuyakamata na asakri wa Tanzania kwa kuwa aliyakuta yakiwa
nchini Kenya ikiwemo kushuhudia makambi yanayotumika kuchoma mkaa na
kusafirishwa nchini humo. Mmoja ya wananchi wa kijiji cha Magojoni
kilichopo wilaya Kwale nchini Kenya Bw. Rumba Dunya alimweleza Mkuu wa
mkoa kwamba wananunua magunia ya mkaa katika kijiji hicho cha Mwakijembe
kati ya sh. 400 na sh. 450 za Kenya ambazo ni sawa na shilingi 8,500 za
Tanzania huku kijiji kikipata ushuru wa sh. 30 za Kenya pindi
wanaponunua magunia hayo ya mkaa.
Diwani
wa kata hiyo Bw. Ramadhani Madika alipopulizwa na mkuu wa mkoa ni
kwanini wanashindwa kuzuia ukataji huo na kuacha rasilimali ya Taifa
ikiendelea kuhujumiwa, alisema kwamba hawawezi kuzuia uhalifu huo wa
ukataji wa miti na uchomaji, kutokana na woga waliokuwa nao wa kuuwawa
na watu wanaojishughulisha na uchomaji huo.
"Mheshimiwa
mkuu wa mkoa, siwezi kuzungumza hapa kutokana na mazingira haya, hii ni
kamati yenu ya ulinzi na usalma na hapa pana watu wengi, lakini
tunaogopa kuuwawaa mimi siwezi kufa kwa kulinda suala hili waacheni
wakate miti, tunaogopa kufa," alisema diwani huyo alisema.
Baada
ya kueleza maelezo hayo mkuu huyo wa mkoa alisema "Kama diwani unaogopa
kufa huwezi kuwa kiongozi jiuzulu basi utoe nafasi kwa watu wengine
wasiogopa kufa kwa kulinda rasilimali za Taifa, ni bora tuitishe
uchaguzi mwingine lakini si wewe uliyeapa kwamba utailinda nchini hii
halafu unasema unaogopa kufa, tena unasema huoni aibu," alisema Mkuu
huyo wa mkoa.
Wakati
Tanzania msitu huo wa Mwakijembe ukiwa unahudhunisha kwa kuvunwa miti
na kupelekwa Kenya kwa ajili ya mkaa na kuchongea vinyago ikiwamo
kusafirishwa magogo nje,msitu huo huo kwa upande wa Kenya msitu
unapendeza kutokana na kuwa na miti yote ya asili na sababu iliyoelezwa
ni kwamba kuna sheria kali ya kulinda maliasili hiyo.
Akiwa
upande wa Kenya,Raia wan chi hiyo walimweleza Mkuu huyo wa Mkoa kwamba,
hawathubutu hata kukata mti mmoja kwenye ardhi yao kwa sababu ya
kuogopa sheria kali badala yake wanaingia Tanzania kuvuna kwa fujo miti
na mkaa na kuuvusha nchini kwao.
Mmoja
wa raia hao wa Kenya ambaye ni dalali wa mkaa unaovunwa katika msitu wa
Mwakijembe upande wa Tanzania,Rumba Dunya alimweleza Mkuu huyo wa Mkoa
kwamba uvunaji kwa msitu huo unafanikishwa kwa kiasi kikubwa na viongozi
wa vijiji vilivyopo Kata ya Mwakijembe ambao hutoa vibali vya uvunaji.
Dunya
ambaye anaishi Kijiji cha Kitongoji cha Mwerere Wilaya ya Kwale nchini
Kenya alisema ndani yam situ huo wa Mwakijembe kuna kambi nyingi za
uvinaji wa magogo ya kuchongea vinyago na mkaa ambazo zinafadhiliwa na
wafanyabiashara waliopo Mombasa.
“Kazi
kubwa ya uvunaji wa miti katika msitu wa Mwakijembe inafanywa na
wananchi wa Tanzania ambao baada ya kuvuna hutayarisha kwa ajili ya
wafanyabiashara kutoka Mombasa kwenda kuchukua shehena kwa shehena na
kisha kuivusha”alisema Naomi Nzuma mkazi wa Kijiji cha Kitwamba Wilaya
ya Kwale.
Wakazi
hao wa Kenya walisema kuwa mkaa unaofikishwa Mombasa hutumika kwa
matumizi ya majumbani lakini shehena nyingi husafirishwa katika nchi za
nje huku magogo yakipelekwa nchi za Uarabuni na Ulaya.
Walisema
gunia moja la mkaa likiwa porini hapo huuzwa kwa bei y ash 6,660 lakini
ukifikishwa katika mji wa Mombasa unauzwa sh 21,600.
“Huku
kwetu Kenya kuna sheria kali ya kutuzuia kuvuna msitu,ndiyo maana
hakuna anayethubutu kukata miti lakini kwa sababu upande wa Tanzania
hakuna sheria ndiyo maana wengi wanakimbilia huko”alisema Naomi
Mkuu
huyo wa Mkoa na msafara wake walisafiri mwendo wa zaidi ya kilomita 300
msituni kukagua yalikowekwa mawe ya kuonyesha alama ya mpaka kati ya
Tanzania na Kenya pamoja na makambi ya kuchomea mkaa na mawe ya mipaka
ambapo pia alikamata maroli yaliyokuwa yakisafirisha bidhaa hizo za
maliasili.
Kufuatia
taarifa alizopata kutoka kwa wakazi wa vijiji vilivyopo upande wa Kenya
,Gallawa aliamuru kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha
Mwakijembe,Francis Mtiambo kutokana na kukaidi amri iliyotolewa na Mkuu
huyo wa Mkoa miezi miwili iliyopia ya kupiga mafuruku utoaji wa vibali
vya kuvuna na kusafirisha mkaa na bidhaa zote za malisili ya misitu.









No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)