MKUU WA MKOA WA RUKWA AFANYA MKUTANO NA WANANCHI WA KATA YA MOLLO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MKUU WA MKOA WA RUKWA AFANYA MKUTANO NA WANANCHI WA KATA YA MOLLO

Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa akizungumza kwenye Mkutano na wananchi wa kata ya Molo ambapo pia wawakilishi wa muwekezaji walialikwa kuskiliza na kutoa kero zao mbele ya wananchi wa kata hiyo. Hata hivyo baada ya Mkuu huyo  wa Mkoa kusikiliza kero hizo aliwaahidi wananchi pamoja na muwekezaji  kuendelea kuushughulikia Mgogoro huo kuanzia ngazi ya Kijiji, Kata,  Wilaya, Mkoa, Wizara na Taifani kwa ujumla kwa ustawi wa wote na  maendeleo ya Mkoa na Nchi kwa ujumla. Alisema kuwa lengo lake sio  kuegemea upande mmoja bali ni kutafuta haki kwa kila pande. Aliwataka  wananchi na muwekezaji kufungua upya milango ya mahusiano mazuri baina  yao ili kumuunga mkono katika kutafuta suluhu ya mgogoro huo ambao  umekuwa ukiibua sura mpya kwa vipindi tofauti.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea kwa ukali wakati  akionyeshwa ramani na Mpima wa Manispaa Selice Nzyungu ya eneo  alilouziwa muwekezaji Ephatta Ministry na lile walilopewa wananchi wa  kata ya Mollo katika Manispaa ya Sumbawanga. Mkuu huyo wa Mkoa  amelazimika kutembelea eneo hilo baada ya kupewa taarifa za awali na  Kamati aliyoiunda katika kufuatilia mgogoro unaoendelea kati ya  muwekezaji na wananchi wanaolizunguka shamba hilo. Lengo kuu la ziara  yake hiyo ya tarehe 02, Septemba 2012 ilikuwa ni kutembelea mashamba  yakiwemo ya muwekezaji na wananchi pamoja na kuzungumza na wananchi na  muwekezaji kwa kuchukua kero zao kwa ajili ya kuutafutia ufumbuzi  mgogoro huo.
 Wananchi wakitoa kero zao mbalimbali zikiwepo unyanyaswaji kwa kuchapwa viboko  na kukatwa maskio kwa pindi wakutwapo na muwekezaji huyo wakipita  shambani kwake au wakikata nyasi kwa ajili ya kulishia mifugo yao. Kero  nyingine waliyoitoa ni kukosa maeneo ya kulima na kupata kipato kutokana na eneo kubwa kupewa muwekezaji ambalo eneo alilopewa ni hekta alfu  kumi (10,000) kwa ajili ya ufugaji kwa mujibu wa Mkataba. Uharibifu wa  barabara pamoja Muwekezaji huyo kwenda kinyume na Mkataba wake wa kufuga na badala kulima zaidi ni kero pia ambayo waliitoa wananchi hao wa kata ya Molo.
 Ndugu Josephat Mutarabuga ambaye ni muwakilishi na mfanyakazi wa Ephata  Ministry Heritage Pharm linalomiliwa na Ephata Minisrty akitoa kero za  muwekezaji huyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambazo ni uharibifu wa  wananchi kwenye shamba lao. Alisema kuwa wananchi wa Vijiji vya  mawenzusi wamekuwa wakichoma moto mashamba yao hali inayopelekea  uharibifu mkubwa wa mazao yao. Alisema pia kuwa wananchi wa vijiji hivyo hukata pia mazao ya mahindi ambayo bado ni mabichi kula Migagi (Kula mashina ya Mahindi kama miwa)
 Wananchi wakitoa kero zao mbalimbali zikiwepo unyanyaswaji kwa kuchapwa viboko  na kukatwa maskio kwa pindi wakutwapo na muwekezaji huyo wakipita shambani kwake au wakikata nyasi kwa ajili ya kulishia mifugo yao. Kero nyingine waliyoitoa ni kukosa maeneo ya kulima na kupata kipato kutokana na eneo kubwa kupewa muwekezaji ambalo eneo alilopewa ni hekta elfu kumi (10,000) kwa ajili ya ufugaji kwa mujibu wa Mkataba. Uharibifu wa  barabara pamoja Muwekezaji huyo kwenda kinyume na Mkataba wake wa kufuga na badala kulima zaidi ni kero pia ambayo waliitoa wananchi hao wa kata ya Molo.
Sehemu ya wananchi, viongozi wa serikali na wawakilishi wa muwekezaji  wakiwa kwenye Mkutano huo uliofanyika tarehe 02, Septemba 2012.
Wawakilishi wa Ephata Ministry wakitambulishwa kwenye Mkutano huo. Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages