Katibu
Mkuu wa CPA Dkt. William Shijja akihutubia wajumbe wa mkutano wa 58 wa
CPA mjini Colombo Sri Lanka, pamoja na kutoa maelezo ya awali kuhusu
shughuli zote za Mkutano huo wa Mwaka. Dk. Shija ni Katibu Mkuu
Mtanzania wa CPA ambaye anatumikia nafasi hiyo kwa kipindi cha pili sasa
tangu 2007.
Spika
wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifuatilia moja wapo ya mada zilizokuwa
zikiwasilishwa wakati wa vikao vya mkutano wa 58 wa CPA Mjini Colombo
Sri Lanka. Pembeni yake ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje
Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu. Waliokaa Nyuma ni
Mhe. Zitto Kabwe na Mhe. Muhonga Said Ruhwanya
Ujumbe
wa Tanzania katika Mkutano wa 58 wa CPA ukifuatilia kwa makini baadhi
ya Mada zilikuwa zikiwasilishwa katika vikao vya Mkutano huo. Wa Kwanza
kushoto ni Mhe. Zitto Kabwe, alieye Kulia ni Mhe. Muhonga Said Ruhwanya
na Nyuma ni Mhe. Hamad Rashid Muhamed ambao wote ni wajumbe wa Mkutano
huo wa CPA kutoka Tanzania
---
Mkutano
wa 58 wa CPA unaendelea leo Mjini Colombo Sri lanka ambapo Tanzania
inashiriki kikamilifu katika kila Vikao na washa mbalimbali za Mkutano
huo. Katika ufunguzi wa warsha hizo ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na
Mhe. Spika Makindaunashiriki mijadala hiyo ikiwa ni pamoja na
kubadilishana uzoefu wa maswala mbalimbali ya Kibunge na wenzao kutoka
Mabunge mengine ya Jumuiya ya Madola.
Hatua
hii inasaidia kupata uzoefu mpya wa uendeshaji wa shughuli za kibunge
ikiwa ni pamoja na kuangalia namna diplomasia ya kibunge inavyoweza
kusaidia mataifa yao katika kushughulikia maswala mbalimbali yenye
changamoto za kidunia
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)