Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaaga walimu kutoka nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano wa 7 wa
ACP, unaojadili kuhusu maboresho ya Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano
huo umefunguliwa leo na Mheshimiwa Makamu wa Rais na unahudhuriwa na
wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika hususani zile
zinazotumia lugha ya Kiingereza katika ufundishaji.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akiwahutubia walimu wakati akifungua mkutano wa siku 3 kwa walimu wa
nchi za Afrika unaojadili kuboresha Elimu kwa nchi za Afrika. Mkutano
huo unahudhuriwa na wawakilishi wa walimu kutoka nchi saba za Afrika
zinazotumia lugha ya Kingereza katika ufundishaji.
Baadhi
ya wawakilishi wa walimu waliohudhuria mkutano huo kutoka nchi za
Afrika leo katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mwakilishi wa Walimu kutoka Uganda, akitoa neno la shukrani.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akitembelea mabanda ya maonyesho katika mkutano huo.
Makamu
wa Rais, Dkt. Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa
Kampuni ya S. Scientific Centre, ambao ni wasamabazaji wa vitabu vya
mashuleni, Shana William, wakati akitembelea mabanda ya maonyesho katika
mkutano huo, leo.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akisoma kitabu katika moja na banda la maonysho katika mkutano huo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na wawakilishi wa walimu kutoka Kenya waliohudhuria mkutano
wa siku 3 wa walimu wa nchi za Afrika kuhusu kuboresha Elimu kwa nchi
za Afrika.
Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Uganda.
Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, akiagana na walimu baada ya kumaliza kufungua rasmi mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)