Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Seif Sharif Hamad, siku ya
Alhamisi tarehe 14/9/12 alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia
maswala ya Afrika Bw. Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao
walibadilishana mawazo kuhusu maswala ya Tanzania na hususan hali ya
kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo hayo yalihudhuria na Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza, Balozi Peter Kallaghe
Makamu
wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akisalimiana na
Viongozi na Wawakilishi wa Jumuiya ya Waingereza walio wahi kuishi
Tanzania (Britain Tanzania Society). Aliyepewa mkono na Mheshimiwa
Makamu wa Rais ni Bwana David Brewin Mhariri wa Jarida la kila mwezi
linalotolewa na BTS, Mama Liz Fennell, Makamu wa Rais BTS (mbele
kulia), Mama Valerie Leach - Katibu (kwanza kushoto), Bwana Dan Coo-
Mwanachama BTS, Bwana Ron Fennel, Afisa wa Miradi ya BTS kwa Tanzania
na Bwana Andrew Coulson, Afisa Mkuu wa Mipango ya Jumuiya hiyo ya BTS.
Makamu
wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, akiwa
pamoja na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki. Mheshimiwa Seif
alikutana na Mabalozi hao jana kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania,
London. Katikati ya picha ni Mheshimiwa, Makamu wa Rais, Balozi wa
Tanzania, Mheshimiwa Peter Kallaghe (kushoto), Balozi wa Rwanda,
Mheshimiwa Ernest Rwamucyo (Pili kushoto), Balozi wa Uganda, Mheshimiwa
Joan Rwabyomere (Pili kulia), na Balozi Mdogo wa Burundi, Mheshimiwa
Bernard Ntahiraja (Kwanza kulia).
--
Makamu
wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mheshimiwa Maalim Seif Hammad, aliendelea
na Ziara yake ya jana hapa nchini Uingereza. Mheshimwa Seif, jana
alikutana na Waziri wa Uingereza anashugulikia maswala ya Afrika Bw.
Mark Simmonds. Kwenye mazungumzo yao walibadilishana mawazo kuhusu
maswala ya Tanzania na hususan hali ya kisiasa ya Zanzibar, mazungumzo
hayo yalihudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,
Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe. Vile vile Mheshimiwa Makamu wa Rais,
aliweza kukutana na Mabalozi wa nchi za Afrika ya Mashariki na Viongozi
wa Jumuiya ya Waingereza waliowahi kuishi Tanzania, ijulikanayo kama
Britain Tanzania Society (BTS).
Leo hii siku ya
Ijumaa, Jioni, kuanzia Saa 18:00pm mpaka saa 21:00, Mheshimiwa Makamu
wa Rais atakutana na Watanzania wote waishio London, katika Ukumbi wa University of London Union, Mtaa wa Malet Street, WC1E 7HY
Watanzania wote wenye nafasi ya kufika mnakaribishwa.
Watakao hudhuria mnaombwa sana kuzingatia muda uliopangwa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)