Kichapo kinaendelea......
Askari huyo akijitahidi kumuwahisha kumuingiza ndani ya geti....
Akifunga
geti baada ya kufanikiwa kumuokoa kutoka katika msiti wa wananchi wenye
hasira kali, huku wananchi hao wakipiga kelele kuwa waachiwe
wammalize...
Askari
wa Kampuni ya Ulinzi anayelinda katika Jengo moja ya benki iliyopo
Barabara ya Bibi Titi eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam, alienda
chini na Kibaka aliyekuwa akimuokoa kutoka mikononi mwa wananchi wenye
hasira kali, baada wananchi hao kuanza kumpa kichapo cha haja baada ya
kibaka huyu kukwapua Ipad katika moja ya gari lililokuwa katika foleni
lililokuwa likiendeshwa na Mwanamama wa Kihindi na kudakwa na mmoja wa
dereva aliyekuwa nyuma ya gari hilo wakati akijaribu kukimbia na
kumuitia mwizi. Baada ya sauti hiyo ya kuitiwa mwizi wananchi
waliitikiwa wito na kuanza kumuandamisha ambapo hakufanikiwa kufika
mbali walimdaka na kuanza kumpa kichapo hadi alipoingilia kali askari
huyo na kumuokoa kisha kumfungia ndani ya geti alilokuwa akilinda.Picha Kwa Hisani Ya Sufiani Mafoto Blog









No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)