
Katibu
wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala (kulia)
akiwakaribisha ofisini kwake wageni kutoka Malawi na Sierra Leone ambao
wako nchini Tanzania kujifunza masuala mbalimbali ya utendaji kazi
yanayofanywa na Tume ya Utumishi wa Umma.

Afisa
Tawala Mkuu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Chele Ndaki akitoa maelezo
ya namna Tume hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa wageni kutoka
Malawi na Sierra Leone ambao wako nchini Tanzania kujifunza masuala
mbalimbali ya utendaji kazi yanayofanywa na Tume ya Utumishi wa Umma.

Katibu
wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Claudia Mpangala (upande wa kulia
katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma
akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Geoigiana Kamara (kulia) kuhusu
utendaji kazi wa Ofisi ya Rasilimali watu ya Sierra Leone.

Naibu
Katibu wa Idara ya Zimamoto na Uokaji, Tume ya Utumishi wa Umma Bw.
Donarld Ndagula (kushoto) akimsikiliza Bw. Abel Mwamlima kutoka Idara
ya Utumishi wa Umma,Sera, Utafiti na Maendeleo kutoka nchini Malawi
(aliyeshika kalamu) wakati wa kikao cha pamoja cha kubadilishana uzoefu
katika shughuli za utumishi wa Umma kati ya Tanzania,Malawi na Searra
Leone.Picha na Aron Msigwa–MAELEZO.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)