Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) akipokea funguo
ya basi la mahabusu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel
Mbonde katika fupi ya kukabidhi mabasi kwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza,
Fidelis Mboya kwa niaba ya Jeshi la Magereza. Programu ya Maboresho katika Sekta
ya Sheria iliyopo ndani ya Wizara ya Katiba na Sheria imetoa magari madogo
matano na mabasi saba kwa ajili ya kusafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda
Mahakamani na kurudi Gerezani. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika leo katika
viwanja vya Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa pili
kutoka kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde (wa
tatu kutoka kulia) wakikagua sehemu ya magari madogo yaliyokabidhiwa na Wizara
ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kusindikiza msafara wa mabasi yanayosafirisha
Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa hotuba
fupi ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla fupi ya kukabidhi mabasi kwa Kaimu
Kamishna Jenerali wa Magereza, Fidelis Mboya kwa niaba ya Jeshi la Magereza.
Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria iliyopo ndani ya Wizara ya Katiba na
Sheria imekabidhi magari 12 kwa Jeshi la Magereza kwa ajili ya kubeba mahabusu
pamoja na kusindikiza msafara wa mahabusu wanapopelekwa mahakamani na kurudishwa
gerezani. Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya Gereza la Keko, jijini
Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa pili
kutoka kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde (wa
tatu kutoka kulia) wakikagua sehemu ya magari madogo yaliyokabidhiwa na Wizara
ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kusindikiza msafara wa mabasi yanayosafirisha
Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakilna Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde wakiwa katika picha ya
pamoja muda mfupi baada ya kukagua sehemu ya magari madogo
yaliyokabidhiwa na Wizara
ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kusindikiza msafara wa mabasi
yanayosafirisha
Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani
IMEANDALIWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO
SERIKALINI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)