Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki akiongea na na wajumbe
wa kamati ya maafa ya mkoa wa Dar es salaam waliokutana leo jijini Dar
es salaam kujadili namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali yanayoweza
kutokea na kusababisha maafa katika jiji la Dar es salaam.
Mkuu
wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema (kushoto) na mkuu wa wilaya ya
Kinondoni Bw. Jordan Lugimbana wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa
zikiwasilishwa kuhusu namna ya kukabiliana na maafa katika jiji la Dar
es salaam leo wakati kamati ya maafa ya mkoa wa Dar es salaam
ilipokutana.
………………………………………….
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Serikali imewataka wananchi
kutopuuza taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kuhusu
athari za mvua kubwa zinazotarajia kunyesha nchini kuanzia mwezi Oktoba
mpaka Desemba 2012 na kuwataka wanaoishi mabondeni kuhama ili kuepuka
madhara ya kukumbwa na mafuriko.
Hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi
ya wananchi wanaoishi maeneo ya mabondeni hususani jijini Dar es
salaam kuupuuza taarifa za wataalam na kukaidi maagizo yanayotolewa na
viongozi wa serikali ya kuwataka kuhama katika maeneo yenye mikondo ya
maji na yale yaliyoainishwa kuwa hatari kwa maisha ya binadamu.
Akizungumza wakati wa kufungua
kikao cha kamati ya maafa ya mkoa wa Dar es salaam kilichowahusisha
wakuu wa wilaya za Temeke, Ilala, Kinondoni pamoja na wataalam wa sekta
ya Afya, Jeshi la Polisi, Kikosi cha Zimamoto na wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na usalama ya mkoa leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa kikao
hicho na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki amesema
mkoa wa Dar es salaam unaendelea kujipanga kuhakisha kuwa wananchi
wanapewa elimu ya namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali.
Amesema kamati ya maafa ya mkoa wa
Dar es salaam imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa shughuli za uokoaji
pindi majanga yanapotokea zinafanyika kwa ufanisi na kuweka nguvu kubwa
katika kuwasaidia wananchi kabla ya tatizo kutokea badala ya kujikita
katika kuokoa wakati wa maafa.
Mwenyekiti amezitaka manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni kuhakikisha kuwa zinatenga maeneo mbadala kwa ajili ya kupeleka na kuhifadhi watu yanapotokea mafuriko na kuwataka kutotumia maeneo ya shule kwa ajili ya kuwahifadhi waathirika.
Mwenyekiti amezitaka manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni kuhakikisha kuwa zinatenga maeneo mbadala kwa ajili ya kupeleka na kuhifadhi watu yanapotokea mafuriko na kuwataka kutotumia maeneo ya shule kwa ajili ya kuwahifadhi waathirika.
“Natoa agizo kwa viongozi wa
manispaa kutenga maeneo mbadala ya kuhifadhi waathirika wa majanga
mbalimbali ili shule ziendelee kutumika kama mahali pa watoto kujifunza,
hata kama shule zimefungwa lazima tutafute maeneo mbadala haiwezekani
tufunge shule wakati maeneo yapo ya kutosha”
Amesema kuna tabia ya baadhi ya
waathirika wanapopewa msaada wa kuhifadhia katika maeneo ya shule
huyatumia kinyume cha utaratibu na wakati mwingine kuharibu miundombinu
na wakati mwingine kugoma kuondoka na kukwamisha shughuli za uendeshaji
wa shule.
Aidha ameitaka kamati ya maafa ya
mkoa wa Dar es salaam kufuatilia mahitaji muhimu ya misaada yatakayokua
yakitolewa wakati wa majanga ili kuwa na akiba na kuepuka usumbufu
unaojitokeza wakati wa tatizo na kuziagiza halmashauri kupitia kwa
wakurugenzi kutenga fedha kwa ajili ya kununulia vifaa vya uokoaji
vitakavyotumika pindi yanapotokea majanga.
‘’Lazima tuwe na ufahamu kutambua
yatakayotokea kwa maana ya kujenga uwezo wa madawa, vifaa vya vya kisasa
vya kuokolea yanapotokea mafuriko,kutenga maeneo maalum na vyumba vya
kuuguzia wagonjwa waliopata madhara mbalimbali” amesema.
Bw. Sadiki amewataka viongozi
wote kuanzia ngazi ya mtaa kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao
kufanya usafi na kuzibua mifereji na kuepuka kutupa taka ovyo ili
kurahisisha maji kutiririka kutoka eneo moja hadi jingine bila kikwazo
chochote.
Kwa upande wake wake Dkt. Meshack
Shimwela kutoka hospitali ya manispaa ya Ilala amefafanua kuwa kufuatia
kuongezeka kwa majanga mbalimbali yanayotokana na vitu vya asili na vile
vya kutengeneza imeundwa timu maalum ya kukabiliana na dharula (DAR
MAERT).
Amesema utoaji wa huduma kwa
waathirika wa majanga mbalimbali umekua ukikabiliwa na changamoto za
ukosefu wa fedha, wataalam na vifaa vya kutosha hasa pale yanapotokea
maafa makubwa.
Naye mganga mkuu wa hospitali ya
Amana Dkt. Christopher Mzava akieleza kwa wajumbe kuhusu mkakati wa
kukabiliana na mafuriko amesema kuwa suala la utupaji wa taka na
uchafuzi wa mazingira limekua chanzo cha kuchangia kuziba kwa mifereji
inayosafirisha maji kuelekea baharini hasa katika jiji la Dar es salaam.
Amesema licha ya changamoto za
kukosekana kwa vifaa vya kutosha vya uokoaji zikiwemo ndege maalum
(Helikopta) jamii inahitaji kuelimishwa kuhusu namna bora ya kukabiliana
na kukwepa majanga.
Kwa kipindi cha miaka mitatu
mfululizo mkoa wa Dar es salaam umeshuhudia majanga mbalimbali yakiwemo
milipuko ya mabomu ya Mbagala iliyotokea mwaka 2009, milipuko ya mabomu
ya Gongolamboto 2012 na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa
zilizonyesha mwaka 2011 na kusababisha upotevu wa maisha, mali na
uharibifu wa miundombinu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)