
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Sei idd akiongoza kikao cha
Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania ambao wao pia ni Wajumbe wa
Kamati hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh.Mohammed
Aboud Mohammed akichangia mada katika Kikao cha Kamati Kuu ya Taifa
yaSensa ya Watu na Makazi kilichofanyika Zanzibar Beach Resort Mbweni.

Baadhi na Mawaziri wa SMT ambao ni wajumbe wakiendelea na Kikao cha
Kamati Kuu ya Taifaya Sensa ya Watu na Makazi hapo Zanzibar Beach Resort
Mbweni--
-
Akitoa Tathmini ya zoezi hilo la Sensa kwa Upande wa Tanzania Bara Waziri wa Fedha wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. William Mgimwa alisema kwa sasa kazi yakuhakiki usahihi na kuhariri taarifa zilizokusanywa na Makarani wa Sensa zinaendelea Nchi nzima kwa kutumia miongozo iliyotolewa na Wizara husika.
-
Kikao cha Nane cha Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi
Tanzania kimekutana leo chini ya Mwenyekiti wake Mweza Makamu wa Piliwa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Hapo katika Ukumbi wa Zanzibar
BeachResort Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Wajumbe
wa Kikao hicho ambao ni pamoja na Mawaziri ,Makatibu Wakuu naBaadhi ya
Maafisa wa Takwimu bara na Zanzibar walipata fursa ya
kutathminimwenendo mzima za zoezi la kuhesabu Watu Nchini Lililomalizika
mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akitoa Tathmini ya zoezi hilo la Sensa kwa Upande wa Tanzania Bara Waziri wa Fedha wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. William Mgimwa alisema kwa sasa kazi yakuhakiki usahihi na kuhariri taarifa zilizokusanywa na Makarani wa Sensa zinaendelea Nchi nzima kwa kutumia miongozo iliyotolewa na Wizara husika.
Dr. Mgimwa alisema wasimamizi katika ngazi ya Taifa, Mikoa na
Wilayawalikuwa na kazi ya kuhakikisha madodoso ya maeneo yote ya
kuhesabia watu katika wilaya zote yameshakusanywa ili kukamilisha awamu
ya pili ya Sensa ya watu na makazi.
Waziri Mgimwa alifahamisha kwamba juhudi za uhamasishaji wa Sensa
Nchini umeonyesha mafanikio kutokana na idadi ya watu waliokataa
kuhesabiwa haikuwa kubwa hasaTanzania Bara.
Alisema Uhamasishaji uliokuwa ukifanyika katika maeneo mbali mbali
nchini kabla ya zoezi la sensa ulilenga kuhakikisha kuwa watu wanapuuza
ushawishi wa kukataa kushiriki sensa ulikuwa unatolewa kupitia
mihadhara ya kidini, vipeperushi, fulana na baadhi ya vyombo vya
Habari.
Dr. Mgimwa alieleza kwamba pamoja na changamoto zilizojitokeza,
juhudizilifanyika kuhakikisha waliolala Nchini Usiku wa kuamkia siku ya
Sensa walihesabiwa na kwamba walitoa Taarifa sahihi zitakazoisaidia
Serikali katikakutunga Sera, kupanga Mipango ya Maendeleo ya Nchi na
kutoa maamuzi sahihi.
Naye
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha, Uchumi na Mipango
yaMaendeleo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Omar Yussuf Mzee
akitoa tathmini kwa upande wa Zanzibar alisema juhudi zinaendelea za
kuimarisha ubora wa kupata idadi ya Watu na kuhakiki madodoso ili kuwa
na Takwimu sahihi kwa maendeleo ya Taifa.
Mh.Omar Yussuf alieleza kwamba ipo haja yakutafutiwa ufumbuzi mambo
yatayoathiri ubora wa takwimu kabla ya kuanza kwa mchakato wa uchambuzi
wa Takwimu hizo.
Wakichangia wajumbe wa Kikao hicho waliwapongeza Makarani,wasimamizi
pamoja na watendaji wote waliosimamia kuendesha zoezi la Sensa yaWatu
na Makazi.
Hata
hivyo walishauri Viongozi wa Serikali zote mbili za Muungano na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhakikisha kwamba changamoto pamoja
na hitilafu zilizojichomoza kabla na baada ya zoezi hilo zisipuuzwe.
“
Baadhi ya wanajamii wetu wamekuwa na Utamaduni wa kutumia hoja
zinazosambazwa na baadhi ya Watu kwa maslahi yao kinyume na muelekeo wa
Taifa”.Alisisitiza mmoja wa wajumbe hao Mh. Mohammed Aboud.
Akitoa
nasaha zake Mwenyekiti Mwenza wa Kikao hicho cha Kamati Kuu yaTaifa ya
Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Balozi Seif Ali Iddi alisema ipo haja
kwa Serikali zote mbili kujipanga vyema katika kutafakari kasoro
zilizojichomoza ndani ya zoezi la Sensa ya watu mwaka huu.
Balozi Seif alisema ipo tabia kwa baadhi ya watu wanaoshawishi
jamiizina zowategemea kuendelea na hulka ya kupinga kila kitu
kinachotolewa au kuagizwa na Viongozi wa Serikali. Wakati huo huo
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na
Mwakilishi wa Jumuiya Aga Khan Foundation aliyepo hapa Zanzibar Bwana
Mohd Baloo.
Katika
mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini
Zanzibar BaloziSeif aliipongeza Jumuiya hiyo yenye Makao yake Makuu
Mjini Geneva kwa dhamira yake ya kusaidia Maendeleo ya Zanzibar hasa
katika harakati za uimarishaji waMji Mkongwe wa Zanzibar.
Balozi
Seif alisema mchango wa Jumuiya ya Aga Khan ndani ya Mji Mkongwe wa
Zanzibar umepelekea ushawishiwa kuwa na mvuto kwa wageni pamoja na
watalii wanaotembelea Zanzibar na hatimaekuongeza mapato ya Taifa
pamoja na ajira kwa baadhi ya Vijana kupitia Sekta ya Utalii.
Mapema
Mwakilishi wa Jumuiya ya Aga Khan Foundation hapa Zanzibar Bwana Mohd
Baloo alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba
Taasisi yake imekuwa ikijihusisha mara kwa mara na ustawi wa Jamii
katika Mataifa mbali mbali Duniani.
Bwana Baloo alisema Jumuiya hiyo bado inaendelea na mipango ya kuongeza
miradi yak eya Kiuchumi itakayosaidia ustawi wa Kiuchumi katika
Mataifa washirika Duniani
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)