KALAMA NYILAWILA FRANSIC CHEKA USO KWA USO JUMAMOSI HII - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

KALAMA NYILAWILA FRANSIC CHEKA USO KWA USO JUMAMOSI HII

Bondia  Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Kalama Nyilawila  litakalofanyika siku ya jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
Bondia Kalama Nyilawila akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Fransic Cheka litakalofanyika siku ya jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.Picha na www.superdboxiongcoach.blogspot.com

MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na aliyekuwa bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni Jumamosi mwaka huu kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila walitwangana mbambanmo wao uliofanyika morogoro ata hivyo ulizua utata baada ya mpambano wao kugubikwa na alama za mshangao ambalo cheka aliibuka na ushindi wa point  mashabiki kuhisika wa mabondia hao wanaogopana na kutafutana kwa mda mrefu watapoza kiu yao kwa mpambano huo jumamosi ya kesho.

Akizungumza Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Oswald Mlay alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa PTA Sabasaba

Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 12 uzito wa kg 72 ambapo leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano uho utakaoamua nani zaidi

Katika Mchezo huo kutakua na Uhuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.
 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages