Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bi Eliwasa Maro akiongea na
Wafanyakazi wa Makumbusho zilizopo Dar es Salaam, pembeni yake ni
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt Paul Msemwa.
Mtawala
Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw Fredrick Mwakalebela, akiongea na
Baadhi ya Wafanyakazi wa Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam wakati wa
kumkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu aweze kongea na wafanyakazi hao.
Pichani
wapili kutoka kushoto ni Dkt Amandus Kweka akufafanua jambo juu ya
Mifupa ya Mijusi (Dinosaur) iliyopo Nchini Ujerumani, wengine ni
wafanyakazi wa Kijiji cha Makumbusho na wa Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni Dar es Salaam.
Na Sixmund J. Begashe wa Makumbusho ya Taifa.
Wafanyakazi wa Makumbusho ya Taifa Nchini wameshauriwa kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya Taasisi.
Hayo
yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Nchini Bi,
Eliwasa Maro alipokutana na wafanyakazi wa Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni Dar es Salaam na wale wa Kijiji cha Mkumbusho kwa lengo la
kujitambulisha kwao na kuwafahamu wafanyakazi wa Makumbusho hayo.
Bi
Maro alisisitiza kuwa ushirikiano, uadilifu na uchapakazi utaisaidia
Taasisi kupiga hatua kubwa kufikia malengo yaliyo wekwa. Ili kufikia
malengo ya Taasisi kila mfanyakazi anapaswa kuitumikia nafasi yake vyema
kwa kutumia ujuzi wa ziada ambapo ana amini kuwa kila mfanyakazi
anauwezo wa kufanya hivyo.
Katika
suala zima la Mawasiliano, Bi Maro aliwataka wafanyakazi wote wafuate
taratibu zinazo stahili za kimawasiliano. Alisisitiza ngazi stahili
zifuatwe na wahusika wakuu watatue matatizo yaliyo chini ya uwezo wao.
Pia
aliwakumbushia wafanyakazi maagizo ya Waziri wa Malihasili na Utalii
Mh Khamis Suedi Kagasheki (MB) aliyoitoa Bungeni wakati akiwasilisha
Bajeti ya Wizara kwamba si vyema kwa mfanyakazi kuvujisha siri za ofisi
kwa lengo la kutaka kutatua matatizo ya Taasisi ama tatizo binafsi bila
kuangalia ukubwa wa madhara yanayo weza kutokea.
Hivyo, Bi Maro alisisitiza umuhimu wa kila mmoja kutathmini maana ya methali “Mvunja nchi ni Mwananchi” katika utendaji wake.
Akizungumzia
suala la Masalia ya Mijusi yaliyo hifadhiwa Nchini Ujerumani, Bi Maro
aliwaomba wataalam wa Makumbusho kutoa elimu ya kutosha kwa jamii
kuhusu masalia ya Mjusi huyo kwani kuna ukweli kuwa watanzania wengi
wana ufahamu mdogo. Alisema kuwa suala hili linahitaji kufanyiwa kazi
kwa kina.
Akitoa
mfano wa ugumu alioupata kusafirisha masalia ya mifupa yenye umri
mdogo wa chini ya miaka milioni mbili toka Nairobi, Mkuu wa Idara ya
Mikusanyo wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Dkt Amandus
Kweka alisema, “Masalia hayo ni mifupa Mawe (Fossil Bones) ya zaidi ya
miaka milioni 200 hivyo usafirishaji wake unahitaji uangalifu mkubwa
kwani ikipata nyufa au kupasuka ni vigumu kuirekebisha na kuwa kwenye
hali yake ya awali” Dkt Kweka pia alisema katika kukamilisha umbo la
mjusi huyo vimeongezwa vipande vya mifupa ya kutengenezwa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofati, baadhi ya wafanyakazi walioudhuria mkutano huo
walimshukuru Kaimu Mkurugenzi Mkuu kwa kukutana nao na kubadilishana
uzoefu na kwa namna alivyoanza kushughulikia matatizo machache makubwa
kwa muda mfupi tangu ateuliwe kukaimu nafasi hiyo.
“Nimefurahi
sana kuona sasa kuna mapinduzi ya kiuongozi katika Makumbusho ya Taifa
kwani ni mara ya kwanza tangu makumbusho yaanzishwe nafasi hii ya Juu
kushikwa na Mwanamke, akina mama tunaweza, si unaona ni muda mfupi
sana tangu Mama Maro ashike nafasi hii na ameleta mabadiliko na
wafanyakazi sasa wana ari ya kazi” alisema Afisa Elimu wa kwanza
mwanamke wa Makumbusho Tanzania,Bibi Lusina Shayo.
Makumbusho
ya Taifa ni Shirika la Serikali lenye wajibu wa kutafiti, kukusanya,
kuhifadhi na kuielimisha jamii juu ya mambo yote yanayo thaminiwa na
jamii.








No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)