Mwasilishaji
wa mada katika jukwaa la Sanaa bwana Chediel Senzighe akisisitiza jambo
wakati akitoa mada kwenye kongamano la Jukwaa la sanaa, jijini Dar es
Salaam jana.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni Tanzania
(CAJAtz) Hassan Bumbuli akizungumza katika Kongamano la Jukwaa la Sanaa
hapo jana.kulia ni msanii Chediel Senzighe aliyekuwa muwasilishaji mada
katika kongamano hilo.
************
Na Mwandishi Wetu
Kongamano
la Jukwaa la Sanaa ambalo huendeshwa kila wiki, jana lilianza kwa
kumkumbuka Mwandishi wa Habari na mwakilishi wa Kituo cha Channel Ten,
Daud Mwangosi aliyefariki dunia juzi katika vurugu zilizotokea katika
kijiji cha Nyololo mkoani Iringa.
Kabla
ya kuanza kwa kongamano hilo jana, Mwendeshaji wa kongamano hilo ambaye
pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na
Utamaduni nchini, (CAJAtz) Hassan Bumbuli aliwataka washiriki kusimama
kwa dakika moja kumkumbuka mwandishi huyo ambaye pia alikuwa mwenyekiti
wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa.
Katika
kongamano hilo ambalo jana lilijadili mada ya Sanaa za jukwaani na
guvu yake katika kufikisha ujumbe kwa hadhira, mwasilishaji wa mada
hiyo Chediel Senzighe kutoka kundi la Jakaya Theatre, aliwakata wasanii
kuandaa kazi kwa kuzingatia maadili na kanuni ili kuepusha kuipotosha
jamii.
“Sanaa
ina nguvu sana katika kufikisha ujumbe, kama ni muuaji basi sanaa
inauwezo wa kuua watu wengi kwa wakati mmoja, daktari akikosea katika
upasuaji ataua mgonjwa mmoja, lakini maudhui ya kazi ya sanaa yakikosewa
yanaathari kwa watu wengi na kwa wakati mmoja. Sasa ni vyema wasanii
tukawa makini katika kuandaa kazi zetu na zaidi tufanye utafiti kabla
hatujaamua kuandaa maudhui ya kazi zetu,” amesema Senzighe.
Wakichangia
mada hiyo, washiriki wa kongamano hilo wamesema tatizo kubwa
linalowakabili wasanii siku hizi ni uvivu wa kusoma na kujifunza na
ndiyo maana wanaandaa kazi za kulipua huku akili zao zikiwaza fedha
zaidi kuliko kufikiria wanachokipeleka kwa jamii kinaweza kuleta athari
gani.
“Wasanii
wetu lazima wabadilike sasa, wafanye utafiti kabla ya kuandaa sanaa
hasa sanaa za jukwaani au filamu hii itasaidia sana kuandaa maudhui
mazuri ambayo pia yataisaidia jamii,” amesema Godfrey Lebejo Mkurugenzi
wa Idara ya Utafiti, mafunzo na habari wa BASATA.
Awali
wakati akifungua kongamano hilo, Katibu Mkuu wa CAJAtz, bwana Bumbuli,
alieleza kusikitishwa na kifo cha kinyama kilichomtokea Mwandishi wa
Channel Ten na kusema matumizi ya nguvu kupita kiasi ya jeshi la Polisi
yanahitaji kukomeshwa mara moja hasa kwa kuwa yanagharimu maisha ya watu
bila sababu za msingi.
“Inatusikitisha
kama wanatsnia ya habari na kama Watanzania, nguvu za polisi zinaacha
majereha makubwa kwa watu na sasa zinagharimu maisha ya watu, nguvu hizi
hazina sababu na lazima zikemewe na kulaaniwa kwa nguvu zote,” amesema
Bumbuli.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)