Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Vipaji maalum ya Ilboru wakipata maelezo jinsi
Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake 21 yanavyofanya
kazi, Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akitoa
maelezo hayo.
Wanafunzi
wa sekondari ya Ilboru wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania kwenye banda la maonyesho wakati wa
mkutano wa 14 wa Mazingira jijini Arusha. Kulia ni Mtaalam wa
Mawasiliano wa UN Sangita Khadka Bista, Harriet Macha kutoka Kitengo cha
Habari cha UN (UNIC) na Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce
Temu.
Meneja
Mkuu wa Uwezeshaji wa Shirika la Manedeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
Bw. Ishmael Dodoo akimwongoza Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr.
Alberic Kacou (wa tatu kulia) alipowasili katika ukumbi wa kimataifa wa
Mikutano (AICC) kuhuduria mkutano wa 14 wa Mazingira na Uzinduzi wa
mtandao wa Mazingira unaosimamiwa na NEMC.
Mratibu
Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (kulia) akisikiliza
Wafanyakazi wa UN Harriet Macha na Katibu wa klabu za Umoja wa Mataifa
mkoa wa Kilimanjaro Angaja Fundisha wakitoa maelezo kwa wanafunzi wa
kike wa shule ya Sekondari Arusha.
Bw.
Ishmael Dodoo wa UNDP wakijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wa
shirika la Umoja wa Mataifa na Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais
Mazingira.
Mratibu
Mkazi wa Umoja Mataifa hapa nchini Dr. Alberic Kacou wakishikana mkono
na kusalimiana na Dr. Mohamed Abdel-Monem wakati wakisubiri kuingia
katika ukumbi wa mkutano wa Mbayuwayu uliopo AICC.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal
(Kulia) akiwa meza kuu na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Muungano wa
Visiwa vya Comoros Dr. Fouad Mohdji (katikati) pamoja na Mratibu Mkazi
wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou wakati wa hafla ya uzinduzi wa
mtandao wa Mazingira wa Tanzania.
Waziri
Afisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akitoa ripoti juu
ya mtandao wa Mazingira utakavyokuwa ukifanya kazi, akifafanua juu ya
mtandao huo na moja ya kazi zake kuwa ni kufikisha kwa wananchi habari
za mazingira juu ya uharibifu na utengenezaji wa mazingira hapa nchini.
Mratibu
Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou akizungumza wakati wa
uzinduzi huo amesema kuwa anaona fahari malengo ya mkutano wa RIO+20
yakifanikiwa na kuyaendeleza mazuri katika kupambana na mabadiliko ya
tabia nchi yanayoendelea kwa sasa kwenye mataifa mbalimbali ulimwenguni
na vilevile Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika mapambano hayo na
kuweza kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilail akiangalia jinsi mtandao wa
mazingira ulivyopangwa na utakavyofanyakazi baada ya kuuzindua rasmi
kwenye ukumbi wa Mbayuwayu mbele ya wataalamu wa Mazingira kutoka nchi
mbalimbali za Afrika na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Mtandao huu unapatikana kupitia www.tanzaniaenviroment.go.tz
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akiteta jambo na mmoja wa wadau wa mazingira kutoka NEMC baada ya kuzindua mtandao huo.
Meza
kuu wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira kutoka
nchi 53 za Afrika kwenye ukumbi wa Simba katika kituo cha mikutano cha
kimataifa cha AICC jijini Arusha.
Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dkt. Alberic Kacou akifurahi
jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Afrika Mashariki Bw.
Abdallah Hamdok.
Pichani
Juu na Chini ni Meza za Mawaziri wa Mazingira barani Afrika na viongozi
wa Umoja wa Mataifa wakati wa uzinduzi wa mkutano 14 wa Mazingira
jijini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Dr. Fouad Mohdji (kushoto)
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira ambaye pia ni Rais wa Mazingira
Barani Afrika kwa kipindi cha miaka miwili Dkt. Terezya Huvisa
(katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo wakifuatilia hotuba
ya ufunguzi kutoka kwa Makamu wa Rais (hayupo pichani).
Waziri
wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan akittoa maelezo
ya mwanzo juu ya mkutano 14 wa mazingira mbele ya Makamu wa Rais
(hayupo pichani) jijini Arusha.
Rais
mstaafu shirikisho la mazingira Afrika (AMCEN) Bw.David Sagara kutoka
Mali akizungumza na mawaziri wa Mazingira na kukabidhi kiti kwa nchi ya
Tanzania ambapo Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya
Huvisa amepokea Urais huo.
Pichani
Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dr.
Alberic Kacou akielezea amesema huu mkutano wao kama Umoja wa Mataifa ni
kuweka misingi na uwezeshaji ambayo inayoletwa na Serikali za mataifa
mbalimbali ambao ni wanachama wa Umoja huo juu ya Suala zima la
maendeleo na mazingira na changamoto zinazoyakibili mazingira na
kusaidia Utawala juu ya swala zima la ardhi ikiwemo misitu kwa ujumla na
kuwawezesha fedha juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na
mazingira kwa ujumla juu ya utumiaji na utunzaji wa mazingira halisia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal
akifungua mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira barani Afrika jijini
Arusha.
Baadhi
ya Wataalamu wa Mazingira wakimsikiliza Makamu wa Rais (hayupo pichani)
wakati akifafanua jambo juu suala zima la mazingira na udhibiti ili
tuendele kuwa mfano na kuapa zawadi nyingine juu ya utunzaji wa
mazingira na gesi ya ukaa ya Ozoni hapa nchini kwetu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)