BANK YA NMB YATOA MADAWATI 160 KWA SHULE YA MSINGI YA ILKONERE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BANK YA NMB YATOA MADAWATI 160 KWA SHULE YA MSINGI YA ILKONERE

Mkuu wa shule ya msingi Ilkonere ,Elihuruma Mollel kulia,akipokea moja ya madawati kati ya 80 yaliyotolewa msaada na benki ya NMB na kukabidhiwa na meneja wa benki hiyo kanda ya kaskazini ,Vicky Bishubo mwishoni mwa wiki katika hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo. Siku hiyo NMB ilikabidhi jumla ya madawati 160 kwa shule mbili za msingi ambazo ni Themi Pamoja na Ilkonere msaada huo unathamani ya shilingi milioni 10.
Meneja wa benki ya NMB kanda ya kaskazini,Vick Bishubo (kushoto)akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Arusha,John Mongela msaada wa madawati 80 yaliyotolewa na benki hiyo kwa shule ya msingi Themi iliyopo manispaa ya jiji la Arusha.
Meneja wa NMB ,Vick Bishubo wa pili kushoto nyuma,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waliofika kuupokea msaada wa madawati,wakwanza kushoto  ni afisa elimu wa manispaa ya jiji la Arusha,Omari Mkongole kulia kwake ,mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongella anayefuata ni mwalimu mkuu wa shule hiyo Zebedayo Mollel na Mwenyekiti wa bodi James Matee pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.
Mahmoud Ahmad Arusha

SHULE mbili za mkoani Arusha zimeondokana na changamoto iliyokuwa ikizikabili ya ukosefu wa madawati baada ya benki ya NMB chini ya mpango wake wa kuendeleza sekta ya elimu hapa nchini, kuzikabidhi msaada wa madawati 160 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10.


Shule hizo ni Themi ya jijini Arusha pamoja na shule ya jamii ya wafugaji ya Ilkonere iliyopo kijiji cha Olmotonyi wilayani Arusmeru ambapo kila moja imepokea msaada wa madawati 80 .


Akikabidhi msaada huo kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki,meneja wa NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo alisema kuwa benki hiyo ilipokea maombi maalumu juu ya uhitaji wa madawati katika shule hizo na baada ya kutembelea alibaini kuwepo kwa changamoto hiyo na ndipo benki ilipoamua kutoa mchango huo.


Alisema kuwa NMB imekuwa na sera ya kusaidia elimu hapa nchini kupitia faida kidogo inayopata kwa kuamua kurudisha sehemu ya faida hiyo kwa wananchi baada ya kubaini uhitaji wa msaada eneo husika, ambapo pamoja na mambo mengine meneja huyo alitoa rai kwa jamii kuona umuhimu wa kuisaidia serikali katika kuporesha elimu hapa nchini.


Aidha alisema kuwa msaada huo ni sehemu tu ya misaada mingi inayotolewa na benki hiyo kwa shule mbalimbali na kuahidi kuendelea kutoa msaada kama huo kwa shule zingine zenye uhitaji huku akiwasihi wanafunzi kujikita zaidi kwenye masomo na kuachana na tabia zisizofaa.


Kwa upande wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ilkonere,Elihuruma Mollel pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa msaada huo,alisema kuwa shule hiyo bado inaupungufu wa madawati 110 ,nyumba za walimu,ofisi ya walimu,Jiko,meza na vyumba 10 vya madarasa.


Naye mkuu wa wilaya ya Arusha,John Mongella ameitaka benki hiyo kutokoma kutoa msaada kama huo kwani umeasidia kwa kiasi kukubwa kwa wanafunzi kusoma vizuri na itasaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.


Aidha alitoa rai kwa wakuu wa shule hizo kuhakikisha kuwa wanatunza msaada huo ili uweze kutumika pia kwa wanafunzi wengine ambao bado hawajaanza shule na kuihakikishia benki hiyo kuwa haitajutia msaada huo kwa shule hizo.


Naye Afisa Elimu wa manispaa ya Arusha,Omary Mkongole alisema kuwa manispaa hiyo yenye jumla ya wanafunzi 57,000 inauhiitaji wa madawati 28,800.
picha zote na Joseph Ngilisho

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages