Meneja
wa Nyanda za juu kusini wa airtel tanzania Bw, Beda Kinunda akipokea
cheti cha heshima toka kwa Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania Dr
Emainuel John Nchimbi wakati wa ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya wiki ya
usalama barabarani mkoani Iringa kwaajili ya kuhamasisha jamii
kuzingatia sheria barabarani katika viwanja vya Samora mkoani hapo
……………………………………….
Maadhimisho ya wiki ya
usalama barabarani yamefanyika Rasmi mkoani Iringa huku maandamano
maalum kwaajili ya kuhamasisha jamii kuzingatia sheria barabarani
yakifanyika katika viwanja vya Samora mkoani hapo.
Katika maadhimisho hayo kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel ilikabidhiwa cheti cha kushiriki na kuwa
wadau wazuri wa usalama Barabarani
Akiongea katika maadhimisho hayo
Katibu Mwenezi wa Usalama barabarani Bw, Heri Bantu ameyataka makampuni
na taasisi mbalimbali kuiga mfano wa kampuni ya Airtel kwa kutoa
mchango wa hali na mali katika kupunguza ajali Barabarani . aidha
amewataka wananchi wote kuwa makini kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za
Usalama Barabarani,
Mara baada ya kukabidhiwa cheti
cha Heshima kwa mchango Airtel Tanzania wamesema wataendelea na kampeni
yao ya kuhakikisha ujumbe wa usalama barabarani “PAMBANA NA AJALI ZA
BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA” unafikia walengwa wote kupitia
njia mbalimbali za mawasiliano
“Airtel Tanzania tunaendelea na
dhamira yetu ya kuhakikisha Usalama barabarani pamoja na kupunguza vifo
vya ndugu zetu kutokana na ajali vinapungua,hivyo tumeanza kutuma ujumbe
mfupi (SMS) kwa wateja wetu nchini kuwasihi kuheshimu sheria barabarani
ili kuokoa maisha ya wengine alisema Mmbando Meneja Mahusiano wa Airtel
Tanzania
Airtel Tanzania ni wadhamini wa
kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani kwa miaka mitano mfululizo
sasa na kwa mwaka huu Airtel imejitolea uchapishaji wa stika za usalama
barabarani pamoja hilo pia Airtel imeshaweka mabango yenye kutoa
tahadhari za barabara kwa abiria na madereva katika barabara mbalimbali
zilizopo nchini kwa lengo la Kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)