Mwenyekiti
wa timu ya Yanga, Yusuph Manji (kulia) Mama Karume (katikati) na baadhi
ya viongozi wa timu hiyo, wakiwa wamepozi wakati wakisubiri utaratibu
wa kuingia katika jumba la Makumbusho ya mauaji ya Kimbari ya mwaka
1994, yaliyotokean nchini Rwanda. Timu hiyo iko nchini Rwanda kwa
mwaliko wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambapo pia itacheza michezo
mitatu ya kujipima nguvu na timu za nchini humo ikiwa ni sehemu ya
mazoezi ya kujiweka sawa na kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu
inayotarajia kuanza Septemba 15, mwaka huu.
Viongozi na wachezaji wa Yanga, wakielekea kuingia katika jumba la Makumbusho ili kujionea makaburi hayo.
Hapa wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maofisa wa Jumba hilo la Makumbusho, kabla ya kuingia ndani.
Viongozi
na wachezaji hao wakiwa na mashada ya maua, wakiinga katika jumba hilo
la Makumbusho kwa ajili ya kuweka mashada ya maua. Picha zote na Saleh Ally
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)