WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA OFISI YA CAG MJINI DODOMA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA OFISI YA CAG MJINI DODOMA

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiweka wa jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya Taifa ya  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mjini Dodoma leo. Jengo hilo jipya lenye urefu wa ghorofa nane,  linatarajiwa kuwa Makao Makuu ya Ofisi hiyo.  
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, wakati alipowasili kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika Jengo hilo leo.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda , akipata maelezo  kutoka kwa Meneja Ujenzi  wa jengo hilo, Casmil Muscbi. Kushoto ni  Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi,  watatu  kutoka kushoto ni  Mwakilishi wa Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Athanas Pius .
 Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Rehema Nchimbi, akishiriki kusebeneka na wasanii wa ngoma za asili, wakati wa hafla hiyo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuweka wa jiwe la msingi katika jengo la Ofisi ya Taifa ya  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mjini Dodoma litakalokuwa na urefu wa ghorofa nane na linatarajiwa kuwa Makao Makuu ya Ofisi hiyo.Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages