Balozi
wa Kinyaji kipya kisicho na kilevi cha Maltiza ambacho kinatengenezwa
na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Sophia Amein (kulia) akimpa kinywaji
hicho mmoja wa wakazi wa jiji la Arusha ili akionje wakati wa uzinduzi
wake uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Sanawari,jijini Arusha.
wakazi
wa jiji la Arusha wakiwa wamejitokeza kwa wingi ili wakionje kinywaji
kipya cha Maltiza ambacho hakina kilevi wakati wa uzinduzi wake
uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Sanawari,jijini hapa.
Wasanii
wa Kikundi cha Hakuna Matata cha jijini Arusha wakitembeza mfano wa
Kinywaji kipya cha Maltiza ambacho hakina kilevi kinachotengenezwa na
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa watu mbali mbali waliofika kwenye
uzinduzi wake uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya
Sanawari,Jijini Arusha.
Kikundi
cha Maonyesho ya Sanaa ya Sarakasi kifahamikacho kwa jina la Hakuna
Matata chenye maskani yake jijini Arusha kikifanya Maonyesho katika
viwanja vya Sanawari,jijini Arusha wakati wa Uzinduzi wa Kinywaji cha
Maltiza jioni ya leo.
Mmoja wa mabalozi wa Maltiza,Lyidia Joseph akiruka kamba sambamba na Wasanii wa Kikundi cha Hakuna Matata.
Mabalozi
wa Kinywaji cha Maltiza wakionyesha umahiri wao wa kulisakata dansi
wakati wa Uzinduzi wa kinywaji hicho uliofanyika jioni ya leo katika
viwanja vya Sanawari,jijini Arusha na kuhudhulia na mamia ya wakazi wa
Jiji la Arusha.
Mdau kutoka TBL akionja kinywaji hicho.
Mamia
ya wakazi wa Jiji la Arusha wakiwa wamefurika katika viwanja vya
Sanawari kushuhudia uzinduzi wa Kinywaji kipya na kisicho na kilevi cha
Maltiza.



















No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)