Ofisi ya Kijiji na Kata ya SINGISA Jimbo la Morogoro Kusini Katika Taswira. Katibu.
Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akionyeshwa madarasa ya
Shule ya Msingi Singisa. Hii ni shule pekee ya katika kijiji hiki
ambacho ni makao makuu ya tarafa na kata ya Singisa.
Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi akionyeshwa sehemu ya
madarasa ya shule ya msingi Singisa ambayo kuta zake zilianguka miaka
miwili iliyopita na mpaka leo hazijakarabatiwa kabla ya kuanza kwa
mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi akiwa na wanakijiji wa
SINGISA jimbo la Morogoro Kusini katika ofisi ya mwalimu wa shule
hiyo.
Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias
Munishi akionyeshwa sehemu ya vyoo vya wanafunzi wa shule ya
SINGISA.Picha Zote na Habari na CHADEMA
---
---
Operesheni
Sangara zinazoendelea Morogoro bado zimeendelea kuwa chachu ya
kuimarisha CHADEMA katika kila vijiji wanavyofikia. Picha hizi ni katika
kijiji ambacho hakuna zahanati na kina shule moja tu ya Msingi yenye
wanafunzi 398 na Mwalimu mmoja tu!!Wanafunzi wote wanakaa chini. Kijiji
hiki ifahamike ndicho pia makao makuu ya tarafa na kata ya Singisa.(Kata
ya Singisa ina vijiji 7). Makao Makuu ya Kata ndipo pia mwisho wa
barabara, hivyo vijiji vingine sita havifikiki na vimetengwa kabisa
kimawasiliano.
Moja
ya lalamiko kubwa la wananchi, wamekuwa wakichangishwa michango isiyo
na idadi na serikali ya kijii huku wakiwa hawasomewi mapato na matumizi.
Baada ya elimu hasa ya uraia na umuhimu wa haki yao hiyo iliyotolewa na
CHADEMA, wanakijiji wameapa ndani ya wiki mbili wataitisha mkutano wa
kijiji na kuwatimua madarakani viongozi wa kijiji baada ya kuenda
kinyume na taratibu za kuendesha serikali ya kijiji.
Hapa
CHADEMA kupitia Katibu Mkuu, BAVICHA Bw. Deogratias Munishi wamezindua
Tawi lenye wanachama 52 na wananchi wamepata fursa kuunda uongozi wao wa
CHADEMA.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)