WAZIRI
wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza amesema kuwa
Tanzania imekubali kuwa mwenyeji wa Jukwaa la Kukuza kilimo katika nchi za Afrika (AGRA), litakalofanyika kuanzia Septemba 26-28.
Akizungumza na wandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo, Chiza alisema kongamano hilo
litafanyika katika mji mdogo wa Ngurudoto, Arusha na kuhudhuriwa na
viongozi wa Kimataifa litajadili sera ya mapinduzi ya kijani.
Alisema Jukwaa katika kongamano
hilo, litajadili na kutafuta njia bora za kuboresha kilimo barani Afrika
na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kwa kushirikiana na vyama vya
ushirika pamoja na wadau wengine.
Chiza alibainisha kuwa mjadala
huo utatoa njia bora za matumizi ya rasilimali na kukabiliana na
changamoto zinazowakabili mamilioni ya wakulima katika bara la Afrika.
“Lengo kuu la serikali ni
kuijenga Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, kwa
kiasi kikubwa na kukua kwa sekta ya kilimo” aliongeza Chiza.
Aidha, kongamano hilo
litawakutanisha pamoja Wakuu wan chi za Afrika, mawaziri, kampuni
binafsi za biashara, kilimo, Taasisi za kifedha na wakulima.
“Wakulima wadogo wadogo ni
kitovu kwa yale tutayafanyayo”alisema Rais wa AGRA, Jane Karuku.
“Mtazamo wetu ni wazi na wakuthibitika, kama sisi tukiwapatia wakulima
wa Afrika dhana za kilimo wanazohitaji watakua zaidi na kuongeza kipato
chao na watatuongoza katika kuelekea mafanikio mazuri.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)