Taarifa ya Utekelezaji wa National Sanitation Campaign (NSC) Upande wa Wizara ya Maji, Kwenye Hafla ya Kusainiwa Participation Agreement ya NSC - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taarifa ya Utekelezaji wa National Sanitation Campaign (NSC) Upande wa Wizara ya Maji, Kwenye Hafla ya Kusainiwa Participation Agreement ya NSC

 Mhandisi Bashiri Mrindoko Naibu Katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya wizara hiyo Ubungo maji  wakati wizara nne zilipotiliana sahihi maafikiano ya utekelezaji wa Participation Agreement ya NSC,  Programu ndogo ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji(WSDP).  Programu hii ndogo inafadhiliwa na Serikali na Washirika wa Maendeleo na kutekelezwa na Halmashauri zote hapa nchini , Wizara zinazohusika na mkataba huo ni  Wizara ya Maji na Umwagiliaji, TAMISEMI, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii
Mhandisi Bashiri Mrindoko Naibu Katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji wa pili kutoka (kushoto)akishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya  utekelezaji huo, wanaosaini kutoka kulia ni Elias Chinamo Mkurugenzi Msaidizi Mazingira, Afya na Maji Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Aelestin GesimbaKaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi na kushoto ni Winfrida Nshangeli Mkurugenzi Uratibu wa Sekta TAMISEMI
--
1.0 Utangulizi
Wizara ya Maji ikishirikiana na wadau mbalimbali inatekeleza Programu ndogo ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji(WSDP).  Programu hii ndogo inafadhiliwa na Serikali na Washirika wa Maendeleo na kutekelezwa na Halmashauri zote hapa nchini zipatazo 132.
Programu hii, ilianza kutekelezwa mwaka 2006. Wakati huo kazi zote zilisimamiwa na Wizara ya Maji. Kazi hizo zilijumuisha utafutaji wa fedha, ujenzi wa miradi mipya na ukarabati wa miradi ya zamani ya maji. Kazi zingine zilikuwa ni uhamasishaji wa Usafi wa Mazingira majumbani na mashuleni.  

Mwaka 2010 Wizara ya Maji na Washirika wa Maendeleo walifanya mapitio ya uendeshaji wa WSDP. Moja ya makubaliano katika mapitio hayo ilikuwa majukumu ya utekelezaji wa kazi za usafi wa mazingira yatekelezwe chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati Wizara ya Maji ikibaki na jukumu la kutafuta fedha na kufanya uratibu wa utekelezaji. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) zinakuwa na jukumu la utekelezaji kwa upande wa mashuleni na Wilayani sawia. 

Fedha za utekelezaji wa Usafi wa Mazingira Vijijini kwa muda wa miaka minne imekadiriwa kuwa dola za kimerekani milioni 20 ambazo sawa na shilingi billioni 30 fedha za kitanzania. Kati ya fedha hizo kiasi cha dola za kimarekani 4.75 milioni ambazo sawa na shilingi bilioni 7.125 fedha za kitanzania zitatolewa na kutumika katika mwaka wa fedha wa 2012/2013.  

Dhumuni kuu la Usafi wa Mazingira Vijijini ni kuboresha Usafi wa Mazingira Majumbani na Mashuleni kupitia mbinu mbalimbali za kuhamasisha jamii juu ya usafi wa mazingira.

Utekelezaji wa mpango huu ndani ya miaka minne umelenga kushawishi kaya 1,300,000 kujenga na kutumia vyoo vilivyo bora. Aidha, jumla ya shule 700 zitafaidika na mpango huo kwa kuwa na vyoo, miondo mbinu ya maji safi na salama na miundo mbinu ya kunawia mikono baada ya matumizi ya choo.

2.0 Hatua za Utekelezaji wa Usafi wa Mazingira Vijijini zilizofikiwa Chini ya Utaratibu Mpya ni kama ifuatavyo:-

    Wizara ya Maji imeratibu zoezi la utayarishaji na kuwekwa saini kwa MOU, ya usafi wa Mazingira kwa Wizara nne (Afya, Maji, Elimu na TAMISEMI)
    Wizara ya Maji imefanya makubaliano ya kupata fedha to Benki ya Maendeleo ya Afrika na Shirika la Misaada la Uingereza la DFID kwa lengo la utekelezaji wa miradi ya Maji na shughuli za usafi wa Mazingira Vijijini.

 Mwezi Machi 2012 Wizara ya Maji ilituma fedha za utekelezaji wa usafi wa mazingira Wizara ya Afya na Wizara ya Elimu kiasi cha shilingi 1.5 bilioni na 1.3 bilioni sawia ili kutekeleza usafi wa mazingira vijijini.

Wizara ya Maji imetoa mafunzo ya mfumo wa kompyuta (MIS) kwa  baadhi ya watumishi wa Halmashauri  na Mikoa yote nchini. Wengine waliyopatiwa mafunzo hayo ni watumishi wa TAMISEMI makao Makuu, Watumishi wa Wizara ya Afya na Wizara ya Elimu. Watumishi waliopatiwa mafunzo hayo ni Wahandisi na Wahasibu. Tarehe 27-31/08/2012 wakaguzi wa ndani toka taasisi zilizotajwa hapo juu watapatiwa mafunzo katika chuo cha Maji Dar es slaam. Lengo la mafunzo hayo nikuboresha upatikanaji wa taarifa za fedha toka taasisi zinazotekeleza Programu.

 
3.0 National Sanitation Campaign Participation Agreement
Kwa lengo la kuongeza kasi ya utekelezaji na kuongeza ufanisi ilikubalika katika vikao vya ndani vya utekelezaji wa program masuala ya usafi wa mazingira yatekelezwe kupitia kampeni ya kitaifa ambayo inajulikana kwa kiingeraza kama National Sanitation Campaign.

Aidha, iliamuliwa ili kuleta uwelewano wa pamoja kwa Wizara husika ni vyema majukumu ya kila wizara ya kaainishwa kupitia Participation Agreement ambayo muda mfupi ujao itasainiwa.


Katika Participation agreement hii majukumu ya Wizara zetu nne ya meainishwa katika kutekeleza program ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira.

Wizara ya Maji itakuwa na majukumu ya fuatayo:-

  Kuratibu masuala ya upatikanaji wa fedha za utekelezaji
Kuandaa viwango ( Standard) vya miundo mbinu ya maji machafu  Kuratibu mpango wa ufuatiliaji na utathimini wa miundo mbinu ya maji machafu

 Kuratibu upatikanaji wa taarifa za utekelezaji usafi wa mazingira toka taasisi zinazotekeleza Programu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Elimu na TAMISEMI


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii itakuwa na majukumu ya fuatayo:-

Kushirikiana na TAMISEMI kuhakikisha malengo ya Participation Agreement yanafikiwa;Kufanya ufuatilaji wa Kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira;

  Kusimamia matumizi ya fedha sawa na makubaliano na Washirika wa maendeleo;
 Kuhakikisha taarifa za matumizi ya fedha zinaingizwa kwenye mtandao wa Kompyuta (MIS);


Kuratibu uandaaji wa taarifa za utekelezaji za robo, nusu na mwaka kamili

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itakuwa na majukumu ya fuatayo:-

  Kushirikiana na wadau wengine kuandaa miongozo ya usafi wa mazingira mashuleni;
        Kufanya ufuatiliaji wa Usafi wa Mazingira mashuleni;

  Kusimamia matumizi ya fedha za usafi wa mazingira mashuleni sawa na makubaliano na Washirika wa maendeleo;

    Kuhakikisha taarifa za matumizi ya fedha zinaingizwa kwenye mtandao wa Kompyuta;
Kuratibu uandaaji wa taarifa za utekelezaji za robo, nusu na mwaka kamili.
 Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa itakuwa na majukumu ya fuatayo:-

  Kusimami utekelezaji wa Kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira katika wilaya zote;
Kuratibu upatikanaji wa msaada wa kiufundi ngazi ya wilaya;
Kuratibu bajeti za Wilaya na Mikoa;

    Kuhakikisha taarifa za matumizi ya fedha zinaingizwa kwenye mtandao wa Kompyuta;
    Kuratibu uandaaji wa taarifa za utekelezaji za robo, nusu na mwaka kamili.

 5.0 HITIMISHO
Baada ya kusainiwa kwa Participation agreement naomba wadau wote tutekeleze majukumu yetu kama yalivyoainishwa ndani ya Participation agreement. Kwa kufanya hivyo tutaweza kufikia malengo ya programu kwa muda muafaka.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages