Mrembo Rahma Jumanne (20)
(katikati) akiwa na warembo wenzake (kushoto) Badria Swale, Susan Robert
(wa pili kulia) ni Everine Manfred na Cesilia Chitanda, wakipozi kwa
‘Snap’, wakati walipokutana kwenye Ufukwe wa Coco Beach wote wakiwa
katika harakati za kupiga picha za mitindo na Movie jijini Dar es Salaam
jana.
Rahma
Jumanne, ni mzaliwa wa Mkoa wa Kigoma, amehitimu masomo ya Msingi
katika Shule ya Msingi Kigoma, na kuendelea na masomo ya Sekondari
katika shule ya Kinyigo na sasa anaendelea na masomo ya elimu ya juu
katika Chuo cha Kampala International College (Information Technology
ICT).
Rahma Jumanne, anapendeea Modelling, Muziki, Movie kusoma habari za kila siku katika magazeti na kusikiliza redio, kusoma Novel
Rahma Jumanne,katika shughuli hizi
za mitindo, anasimamiwa na Kampuni ya Next Logistics, ili aweze kufikia
malengo yake na kuonyesha kipaji chake katika mitindo na mavazi. Mrembo
huyu hivi sasa anafanya kazi za ICT na kampuni ya Poa Technology Ltd,
akiendelea kujipanulia wigo wa ujuzi na elimu katika masuala ya ICT,
katika chuo cha Kampala kilichopo jijini Dar es Salaam. Picha zote na www.sufianimafoto.blogspot.com
MDAU WA MITINDO NA UREMBO UKIHITAJI KUSHIRIKI NAYE WASILIANI NA MTANDAO HUU SIMU ZILIZOPO KATIKA UKURASA HUU. www.sufianimafoto.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)