Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na
Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Radegunda Maro, wakati ofisa huyo
alipofika nyumbani kwa Makamu akiwa na Karani wa Sensa na msimamizi wake kutoka
Kituo cha Oysterbay, kwa ajili ya kukamilisha zoezi la Sensa, leo asubuhi
Agosti, 26, 2012
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akijiandaa kujibu maswali kutoka kwa Karani wa Sensa, Happyness Masaka (kulia)
ikiwa ni sehemu ya kukamilisha zoezi hilo la Senza ya watu na Makazi,
lililoanza leo nchini kote, ambalo
litadumu kwa siku saba
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Karani wa Senza, Happyness Masaka, baada ya kukamilisha zoezi la
kujibu maswali husika katika zoezi hilo, leo asubuhi nyumbani kwake Oysterbay,
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msimamizi wa Sensa wa Kituo cha Oysterbay, Daria
Kailembo (kushoto) ni Ofisa kutoka Ofisi ya Takwimu ya Ttifa, Stanley Mahembe.
Picha na OMR
MAKAMU wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo Agosti
26, saa tatu asubuhi, ameshiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya watu na Makazi
akiwa kwenye Makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Dkt. Bilal,
ameshiriki katika zoezi hilo kwa kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Karani
wa Kituo cha Oysterbay, Happyness Masaka, mbaye alifika nyumbani kwa makamu
akiwa ameongozana na msimamizi wake, Daria Kailembo, pamoja na Maofisa kutoka
Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Stanley Mahembe na Radegunda Maro.
Aidha, Dkt. Bilal, ametumia dakika 25 kwa kujibu jumla ya maswali 37,
yaliyoandaliwa ili kukamilisha zoezi hilo.
Akizungumza
baada ya kukamilisha zoezi hilo, Dkt. Bilal, amewahasa Watanzania wote kwa
ujumla kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa Makarani ili kufanikisha zoezi hilo,
ambalo litadumu kwa siku saba.
Imetolewa
na Ofisi ya Makamu wa Rais
Box 5380 Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)