Ndugu Waandishi,
Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba hata
mimi nimeshiriki katika vitendo vya rushwa, kwa nafasi yangu kama
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma. Taarifa hizo, kama
kawaida ya uzushi mwingine wowote zimesambazwa kimkakati na kwa kasi
kubwa kiasi cha kuukanganya umma.
Nafahamu
nabeba dhamana kubwa ya uongozi, taswira yangu ya uongozi daima
imeakisi njozi na matumaini ya wananchi wa Kigoma Kaskazini, wananchi
wanyonge na vijana kote nchini bila kujali itikadi zao za kisiasa,
jinsia zao, makabila yao na rika zao. Hivyo, nawajibika kupitia kwenu
kuwatoa hofu juu ya hisia potofu zinazopandikizwa kwao na wale
wasiopenda kuona baadhi yetu tukiwaunganisha na kuwasemea watanzania
wasio na sauti, dhidi ya vitendo vya hujuma na vyenye dhamira ovu kwa
taifa.
Mkakati huo wa kuniunganisha na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wanaotuhumiwa kwa kupokea Rushwa unatekelezwa kwa njia zifuatazo:
- Kumekuwa na kauli za watendaji wa serikali ambao wamekuwa wakizieneza na hususan kutoa taswira kwamba baadhi ya kauli zangu zinatokana na ushawishi wa rushwa;
- Kuna taarifa ambazo zimeandikwa tena katika kurasa za mbele za baadhi ya vyombo vya habari zikidai ’’Zitto kitanzini’’ ama ’’Zitto sawa na popo nundu’’ zikiashiria kwamba na mimi ni mla rushwa; na
- Waandishi wa habari na jamii kwa ujumla wamefikia kuaminishwa habari hizi kiasi cha wengine kuuliza kwa nini Mhe. Zitto Kabwe hakutajwa katika orodha iliyotolewa na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani.
Ndugu Waandishi,
Naomba
kutoa ufafanuzi wa hicho kinachoelezwa kwamba nina ushiriki katika
masuala ya rushwa hususan kwenye masuala yanayohusu sekta ya Nishati na
Madini:-
- Mara baada ya bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Usambazaji wa Umeme Tanzania (TANESCO) chini ya Uenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Robert Mboma kutangaza kwamba imemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Nd. William Mhando ili kupisha uchunguzi wa baadhi ya vitendo/mwenendo wake, Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ambayo mimi ni Mwenyekiti wake ilimuandikia Mhe. Spika kumuomba aridhie ili Kamati iweze kuwaita Bodi ya TANESCO, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali (CAG) na pia Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kujiridhisha na tuhuma zote zinazotajwa zinafanyiwa uchunguzi wa kina na hatua kuchukuliwa Kwa Kusoma Zaidi Bofya Hapa
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)